Michuano ya Euro 2016 imeendelea kama
kawaida June 16 2016, michuano inazidi kuwa migumu kutokana na timu
kuingia katika round ya pili ya hatua ya Makundi, hivyo zinahitaji point
ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi, June 16 imechezwa michezo
mitatu, lakini mchezo kati ya Ujerumani dhidi ya Poland ulionekana kuwa
mgumu zaidi.
Katika mchezo wa Ujerumani dhidi ya
Poland umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya 0-0, hivyo kutokana na
timu hizo michezo yao ya kwanza ilipata ushindi, zote zinakuwa
zimetimiza point nne ila Ujerumani anaongoza Kundi C kwa tofauti ya
magoli, wakati Ukraine kutokana na kutokuwa na point hata moja,
wanasubiri kukamilisha ratiba.
Baada ya matokeo hayo hii inakuwa
fainali ya tano kubwa kwa timu ya taifa ya Poland kushindwa kupata
ushindi mbele ya timu ya taifa ya Ujerumani, Mario Gotze na Mesut Ozil
walionekana kupata nafasi amabazo wangeweza kuipatia ushindi Ujerumani,
ila golikipa wa Poland Lukasz Fabianski alionekana kuwa imara kwa kuokoa
hatari zote golini.
Post a Comment