Baraza la madiwani la wilaya ya kondoa limeazimia kusimamishwa kazi kwa
wakuu wa idara wanane kwa upotevu wa shilingi milioni 180 huku
wakimuandikia barua waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na
serikali za mitaa mhe george simbachawene wakimtaka amrudishe aliyekuwa
mkurugenzi wa halmashauri hiyo isdory mwalongo ili ahojiwe wakimtuhumu
kuwa ndio muusika namba moja wa upotevu huo.
Akisoma maazimio hayo ambayo yalitokana na Baraza hilo kukaa kama kamati na kujadili upotevu huo wa pesa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kondoa Omary Kariati amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya madiwani kuridhia wakuu hao wa idara kusimamishwa huku ikibainika aliyewahi kuwa Mkurugenzi Bwana. Mwalongo katika upotevu huo shilingi milioni 34 amesaini hundi yeye mwenyewe.
Wakizungumza baada ya kufikiwa kwa uamuzi huo baadhi ya madiwani wamesema wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuchoshwa na vitendo vya ubadhilifu wa fedha katika halmashauri hiyo ambapo watumishi wake waliigeuza shamba la bibi huku pia ikinuka rushwa na dhuluma.
Awali katika baraza hilo mkuu wa wilaya ya Kondoa Shaaban Kisu amezungumzia changamoto mbalimbali zinazoikabili wilaya hiyo ambapo maeneo ambayo yamekuwa na matatizo kwa muda mrefu ni kwenye migogoro ya ardhi na uharibifu mkubwa wa Mazingira.

Post a Comment