Timu ya kidato cha nne ambao leo septemba 30 wameweza kutoa dozi ya magoli 2-0
Timu ya kidato cha sita ambao leo septemba 30 wamekubali kichapo cha magoli 2-0
Timu ya kidato cha nne wamekuwa mabingwa wapya katika ligi ya mbuzi baada ya kuwasambalatisha timu ya kidato cha sita magoli 2-0
Fainali ya Ligi ya kugombea mbuzi (mnyama) imepigwa leo septemba 30 katika uwanja wa shule ya sekondari
liwale day (Liwale High School) iliyopo wilaya ya Liwale mkoani Lindi, mchezo uliwakutanisha wasomi wanaotarajia kuweka histori shuleni hapo kati ya timu ya kidato cha nne (iv) dhidi kidato cha sita (vi).
Katika mchezo huo wa fainali timu ya Kidato cha nne waimebuka
kidedea kwa kuwafunga kidato cha sita bao 2-0. Magoli yamefungwa na
shadhili kimbowe na goli la likifungwa na Jamali mkopora.
Mbwembwe za mashabiki wa timu ya kidato cha nne ambao ndio mabingwa wapya ligi ya mbuzi mwaka huu Mashabiki wa timu ya kidato cha sita wakishangilia kiana yao lakini waliambulia kichapo cha magoli 2-0
Post a Comment