Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe
Magufuli, leo tarehe 30 Septemba, 2016 amefunga maadhimisho ya miaka 52
ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kushuhudia zoezi la medani
liitwalo ''Amphibious Landing'' lililofanyika katika Kijiji cha Baatini Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Zoezi
hilo lililochukua muda wa wiki mbili, limeshirikisha kamandi zote tano
za JWTZ ambazo ni Nyika, Majini, Anga, Kamandi ya Makao Makuu na Jeshi
la Kujenga taifa limefanyika katika ufukwe wa bahari ya Hindi na
limetekelezwa kwa mfano wa mapambano ya kivita yaliyohusisha kutua nchi
kavu kutoka majini na kukomboa eneo
lililotekwa.
lililotekwa.
Akizungumza
baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Rais na Amiri jeshi Mkuu Dkt.John
Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis
Mwamunyange pamoja na Makamanda na Wapiganaji wote wa JWTZ walioshiriki
katika zoezi hilo ambalo limefanywa kwa umakini, uhakika na weledi wa
hali ya juu.
''Kwa
kweli nimefurahi na nimeamini tuna wapiganaji wa kutosha katika maeneo
yote, hii mikakati na mipango iliyotumika inaonesha tuna jeshi imara na
linaloaminika'' amesema Dkt. Magufuli.
Rais
na Amiri Jeshi Mkuu amewahakikishia Makamanda na Wapiganaji wote wa
JWTZ kuwa Serikali yake itahakikisha inaendeleza na kuongeza zaidi
juhudi zilizofanywa na Marais waliopita kwa kuimarisha na kuwa na jeshi
la kisasa linalotumia vifaa na
teknoljia ya kisasa na pia itahakikisha maslai ya askari yanaboreshwa.
teknoljia ya kisasa na pia itahakikisha maslai ya askari yanaboreshwa.
Aidha,
Dkt. Magufuli ametaka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuimarishwa zaidi na
kujielekeza katika uzalishaji mali ikiwemo uwekezaji katika viwanda. Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ambaye pamoja na kuipongeza JWTZ amesema miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo Watanzania wanashuhudia jeshi lao likiwa imara na makini zaidi kwa ajili ya kulinda nchi.
Nae
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amemshukuru Rais
na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake na nia
yake ya kuliimarisha Jeshi na kuboresha maslai ya Makamanda na
Wapiganaji na ameongeza kuwa anajivunia kuwa kiongozi wa Jeshi hilo.
Maadhimisho
hayo yamehudhuriwa na Viongozi wengine wakiwemo Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Abdulhamid Yahaya
Mzee.
Rais
na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, amemuagiza Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kuwapa ajira za JWTZ askari
mgambo wote walioshiriki zoezi la Amphibious Landing.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
30 Septemba, 2016
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akipiga ngoma za bendi ya
jeshi ya Mwenge Jazzz wana Paselepa wakati wa kufunga Zoezi la medani
katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba
30, 2016
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali
Mohamed Shein na meza kuu wakipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa
wakati wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka
52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini,
Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
Ndege
vita zikipita angani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa
Pwani leo Septemba 30, 2016
Vifaru
vinavyopita baharini na nchi kavu vikiwa katika zoezi la "Ambhibious
Landing" katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo
Septemba 30, 2016
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali
Mohamed Shein na meza kuu wakipiga makofi wakati wa Zoezi la medani
katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba
30, 2016.PICHA NA IKULU.
Post a Comment