wameandamana
kwa kufunga barabara na kumpiga mfanyakazi wa shirika la ugavi wa umeme
Tanesco wakilalamikia shirika hilo kupitisha nguzo za umeme kwenye
mashamba yao kupeleka nishati hiyo katika vijiji jirani bila wao
kupatiwa huduma hiyo.
Wakizungumza
kijijini hapo wananchi hao wamesema wameamua kuandamana na kufunga
barabara kufuataia shirika la umeme Tanesco kushindwa kusambaza huduma
hiyo katika kijiji hicho na badala yake kupitisha nguzo katika maeneo
yao kupeleka huduma katika vijiji vya jirani ambapo wamesema
hawapotayari kuruhusu mradi huo kuendelea hadi watakapohakikishiwa
kuunganishiwa nishati hiyo.
Nao
viongogozi wa kata na kijiji cha Lumuma wamesema wanaunga mkono wananchi
kwani wamesema inaonekana zoezi hilo limegubikwa na hujuma huku
wameomba serikali na uongozi wa Tanesco kuona uwezekano wa kuanza
kusambaza umeme katika kijiji cha Lumuma na badaye kumalizia katika
vijiji vilivyoko katika kata hiyo.
Akiongea
na ITV kwa njia ya simu meneja Tanesco mkoa wa Morogpro Mhandisi John
Bandiye amesema anatambua kuwepo mradi wa umeme katika kata ya Lumemo
lakini hafahamu kama wananchi wa kijiji hicho wanalalamika na kwamba
atafuatilia ili kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.
Post a Comment