Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na viongozi wa vyama vyote nane
imesema wametangaza uamuzi huo baada ya kutokuridhishwa na maamuzi ya
tume ya uchaguzi Zanzibar chini ya uenyekiti wa Jecha Salim Jecha.
Mwanasheria wa vyama hivyo Bw Ally Omary Juma amesema sheria No 5
ya mwaka 1992 ya bunge la Tanzania inayoruhusu uanzishwaji wa vyama vya
siasa ni muhimu ikazingatiwa.
Licha ya CUF kutangaza mapema kutokushiriki uchaguzi huo vyama
vingine vilivyotangaza kutokushiriki uchaguzi huo ni pamoja na ACT
Wazalendo, Jahazi Asilia, Chauma, SAU, NRA, UPDP na UMD.
Post a Comment