Mamlaka
ya chakula na dawa TFDA kanda kati wameteketeza tani za vipodozi, vifaa
tiba na vyakula vyenye uzito wa tani tatu nanusu zikiwa na thani ya
shilingi milioni kuminatatu na laki tano ambazo hazitakiwi kutumika
nchini na vilivyo kwisha muda wake wa matumizi.
Akiteketeza vifaa hiyo afisa mkaguzi wa chakula kutoka mamlaka ya
chakula na dawa TFDA kanda ya kati Bwana Aberl Deule amesema baadhi ya
wafanyabiashara sasa wameanza kubadilisha muda wa matumizi kwenye bidhaa
za makopo na kusababisha wananchi kupata madhara ya kuugua matumbo.
Kwa upande wake mganga mkuu wa manispaa ya Singida Daktari John
Mwombeki amesema pamoja na wafanyabiashara wengi kufahamu madhara ya
kuuza bidhaa za vipodozi ambvyo vimekatazwa hapa nchini na kupunguza
kasi ya kuvileta tofauti na awali, sasa wamekuwa wakitumia njia ya
kuzificha bidhaa hizo tofauti na awali walikuwa waki viweka katika mbao
za kuuzia.
Mamlaka ya chakula na dawa kanda ya kati TFDA imefanya operationi
hiyo kwa muda wa siki kumi katika kata nane na kukagua majengo miamoja
themanini na tatu yakiwemo majengo ya dawa viwanda vya chakula na
machinjio ya manispaa ya Singida.
Post a Comment