Marcus Rashford kwa mara nyingine tena amekuwa Shujaa wa Manchester United kwa kuwafungia Bao 1 na la ushindi walipoifunga Celta Vigo 1-0 waliokuwa kwao Estadio Balaidos kwenye Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UEFA EUROPA LIGI.
Celta Vigo, ambao wako Nafasi ya 11 kwenye La Liga, wamekuwa wakinyanyasa Timu nyingi hapo kwao Estadio Balaidos wakiwemo Mabingwa wa Spain Barcelona ambao kwenye Mechi ya mwisho walinyukwa 4-3.
Wakikosa nafasi nyingi za kufunga, Man United walifunga Bao lao Dakika ya 67 kwa Frikiki ya Marcus Rashford ambayo ilimhadaa Kipa wa Celta Vigo Alvarez alietegemea Daley Blind atapiga lakini akauruka Mpira na Rashford kuupinda wavuni.
Timu hizi zitarudiana tena Alhamisi ijayo katika Dimba la Old Trafford.
VIKOSI:
CELTA VIGO: Alvarez; Mallo [Beauvue 92], Cabral, Roncaglia, Jonny; Wass [Sánchez Ruiz 74], Radoja, Hernandez; Aspas, Sisto, Guidetti
Akiba: Villar, Fontas, Diaz, Bongonda, Beauvue, Jozabed, Gomez
MAN UNITED: Romero; Valencia, Bailly, Blind, Darmian; Herrera, Pogba, Fellaini; Lingard, Rashford [Martial 80], Mkhitaryan[Young 78, Smalling 89]
Akiba: De Gea, Mata, Martial, Smalling, Carrick, Rooney, Young
REFA: Sergei Karasev (Russia)
Post a Comment