0






Wawakilishi wa wakulima walioudhulia kwenye bei ya mnada uliofanyika leo octoba 30 wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
 Meneja mkuu wa Chama kikuu cha Ruangwa,Nachingwea na Liwale (RUNALI), Christopher H. Mwaya (kushoto) akifungua barua za tenda mbele ya wakulima wilayani Liwale.
wakulima wa zao la korosho wakifuatilia mnada wa bei ya korosho uliofanyika leo hapa wilayani Liwale.

LIWALE-LINDI. Kwa mara ya kwanza wakulima wa korosho mkoani Lindi, wameuza zao hilo kwa mnada na kupata bei kubwa ya Sh3,740 kwa kilo moja ya korosho ghafi badala ya Sh 2,400 za msimu uliopita.

Mnada wa kwanza wa wazi umefanyika leo octoba 30  katika viwanja vya mikutano kwa Nanjinji katika kijiji cha Likongowele kata ya Likongowele wilayani Liwale.


 Katika mnada huo katika ghala kuu la chama cha ushirika cha msingi umoja wilayani Liwale kuna jumla ya kilo za korosho 408,939 na wakulima walikubalia zitanunuliwa kwa bei ya shilingi 3710 baada ya kampuni moja kushinda tena ya kununua idadi za kilo zote zilizopo.


Ghala la Nachingwea kuna jumla ya kilo za korosho 2,658,777 zitanunuliwa kwa bei kati ya shindi 3740-3700 baada ya kupata kushindi wa tenda kwa kampuni 8 kufikia kununua idadi ya kilo zote zilizopo.


Katika mnada huo, wakulima walishuhudia bei zikishindanishwa kampuni 17 zilizoomba kununua korosho, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali kutaka wakulima kushirikishwa katika mnada.

Meneja mkuu wa Chama kikuu cha Ruangwa,Nachingwea na Liwale (RUNALI), Christopher H. Mwaya alisema waliamua kufanyia mnada wa wazi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali la kutaka wakulima wa korosho washirikishwe katika minada.

Meneja mkuu wa Runali Christopher H. Mwaya alisoma barua zote za kuomba zabuni ya kununua korosho zilikuwa za siri, zilisomwa mbele ya wakulima na mwisho walichagua kampuni iliyotangaza bei kubwa kuliko.

“Tumetekeleza agizo la Serikali la kufungua minada katika wilaya, wakulima wameshiriki na kufanya maamuzi, kwa maana hiyo utaratibu huu ni mzuri kwani unatoa fursa kwa wananchi na viongozi kuona na kushiriki moja kwa moja" alisema Mwaya.

Mkaguzi Mwandamizi wa bodi ya korosho,Christopher A. Mwaya alisema wakulima wa wilaya ya Liwale wanatakiwa kupeleka korosho zao kwenye maghala kwa wakati kabla ya kipindi cha mvua kutokana na miundombinu ya barabara si mizuri inaweza ikaathiri bei ya korosho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Umoja  Amcos pia Makamu mwenyekiti wa Runali,bwana Hasani Mpako aliwataka wakuluma kupeleka korosho boro ili kulinda thamani ya ubora wa korosho za Liwale na thamani ya bei ya mnada iliyopo sasa aliongeza kusema kama wakulima watapeleka ghalani korosho zisizo na ubora zitaathi bei za korosho zote hapa wilayani.

Mkurugenzi wa Halmshauri ya Liwale,Justin Monko alisema kufanyika kwa mnada huo mbele ya wakulima na viongozi utasaidia kuondoa malalamiko yasiyo ya lazima na amewataka kupeleka korosho zao kwenye maghala kwa wakati na kuacha kuuza korosho zao kwa walanguzi.

Baadhi ya Wakulima walitoa maoni  yao juu ya huwalikishaji wa malipo mara baada ya kununuliwa kwa korosho zao.

Post a Comment

 
Top