AFISA Mfawidhi wa Forodha Bandari ya Tanga Zahor Makame akizungumza katika mkutano huo
MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo kushoto akiwa na Kaimu Meneja wa TRA Mkoani Tanga Nazarius Mfikwa wakifuatilia kwa umakini hoja za wananchi wa kijiji cha Kigombe leo
Mkazi wa Kijiji cha Kigombe Kata ya Kigombe wilayani Muheza mkoani Tanga Tajiri Twaha akiuliza swali kwenye mkutano
WANANCHI wa Kijiji cha Kigombe Kata ya Kigombe wilayani Muheza mkoani Tanga wametakiwa kuacha kushiriki kwenye biashara za magendo badala yake watumie maeneo yaliyorasmi kwa kisheria kwa ajili ya upitishaji wa bidhaa.
Wito huo ulitolewa leo na Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo wakati akizungumza na wananchi hao kwenye mkutano uliofanyika kwenye eneo la sokoni akiwa ameambatana na maafisa wa TRA mkoa wa Tanga.
Alisema kitendo cha wananchi kuacha kutumia bandari ya Pangani ambayo ipo kusheria wanafanya makosa makubwa na kuwataka kuitumia kupitisha bidhaa badala ya kutumia zile ambazo hazitambuliki ambazo watakapokamatwa watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria.
“Tumefika hapa kigombe kutoa elimu kwa kuzungumza na wananchi kutokana na changamoto za mara kwa mara biashara za magendo ambazo zimekuwa zikipitishwa eneo hilo na kuona kutumia muda huo kuzungumza na wananchi kuwaambia madhara yake ni yapi”Alisema.
Aidha alisema kuwa katika eneo hilo ambalo lipo kilomita 10 kutoka wilayani Pangani ambako kuna Bandari rasmi waendelee kuitumia hiyo na kuchana na matumizi ya bandari bubu ya Kigombe kwani kuendelea kuitumia wanakuwa wakivunja sheria zilizopo
Pia aliwataka wananchi hao kupitisha bidhaa zao kwenye Bandari za Tanga na Pangani ambazo zipo kisheria ili bidhaa zao ziweze kuhakikiwa ili walipwe ushuru ikiwemo kuepukana na kukimbizana na gharama kubwa wanazoingia kukumbizana na wafanyabiashara za magendo.
Hata hivyo alisema hivi sasa chombo cha baharini, nyumba ambazo zitakutwa zimehifadhiwa bidhaa za magendo zitataifishwa ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha biashara za namna hiyo zinakwisha kwenye jamii na hivyo kumfanya kila anayeingiza bidhaa kutumia maeneo yaliyopo kisheria.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Post a Comment