Leo imekuwa siku ngumu sana kwa uchukuzi mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Kisa na maana,,,,mafuriko. Wenyeji walitatazikika kuendesha shughuli zao za kawaida
Baadhi ya barabara kuu za kitovu hicho cha kibiashara cha Tanzania, zilikuwa hazipitiki. Maji kila mahali
Mvua kubwa inayoendelea kunyesha hivi sasa kanda
yote ya Afrika Mashariki imesababisha mafuriko makubwa ambayo muundo
msingi wa barabara za miji ya Nairobi na Dar es Salaam haziwezi kumudu.
Magari ambayo yalijaribu kutumia mabarabara ya Dar es Salaam yalikwama mengine huku yale yenye kimo cha juu yakifaulu kupita. Magari mengi yamekwama barabarani
Wenyeji sasa wameanza kuhoji uwezo wa muundo msingi
wa maji taka wa mji huo wa Dar es Salaam hususan ukizingatia kuwa ndio
sasa msimu wa mvua umeanza.
Mtangazaji wetu wa Dar es Salaam Sammy
Awami amefaulu kuondoka nyumbani kwake na katika pita pita zake
ametutumia picha hizi zinazoonesha hali halisia ya baadhi ya mabarabara
ya Dar es Salaam. Wenye magari mjini Nairobi wataabika mabarabarani
Nchini Kenya hali sio tofauti.
Barabara ya kisasa ya Thika Super Highway haipitiki baada ya mvuo kubwa kunyesha mchana na kusababisha mafuriko makubwa. Mtabiri wa hali ya hewa anasema mvua bado inatarajiwa
Kinaya ni kuwa mtabiri wa hali ya hewa anasema kuwa mvua kubwa inatarajiwa kunyesa mjini Nairobi na maeneo mengi ya nchi.
Wenyeji
wa mji huo wa Nairobi wameanza kutoa hasira zao kwenye mitandao ya
kijamii wengi wakipiga picha maeneo yaliyokumbwa na mafuriko.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wasikubali kuchonganishwa na kwamba Serikali haiongozwi kwa misingi ya kidini bali imeziachia ta...Read more »
MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kigom...Read more »
Mshehereshaji wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi, Mtafiti mshiriki wa ESRF, Abdallah Henku aki...Read more »
Polisi mkoani Morogoro, wameanza upelelezi wa tukio la mwanamke mmoja, Amina Mbunda kujifungua nje ya kituo cha Polisi, Mang’ula Morogoro baada ya...Read more »
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.