0


Papai husaidia kuyeyusha chakula mwilini kutokana na kuwa na kimeng'enya kiitwacho 'papain'. Tunda hili pia lina vitamin A na C (antioxidants). Mbali na faida hizo kwa mwili wa binadamu tunda hilo pia ni tiba kwa magonjwa mbalimbali. Mathalani, mbegu za papai hutibu kuharisha (dysentery) na minyoo kwenye njia ya mfumo wa chakula (gastrointestinal tract). Pia mizizi ya papai hutibu gono (gonorrhea).

Kadhalika watu wanaosumbuliwa na maumivu ya viungo (Arthritis) na magonjwa au matatizo mengine kama mzio (allergy) asthma, hypertension, maumivu ya jino, na watu wenye tatizo la kupatwa na wasiwasi (chronic anxiety), tatizo la kinga ya mwili kuwa ndogo (low immunity), mwili kukosa nguvu, na uchovu (chronic fatigue) wanashauriwa kula papai kila siku au mara kwa mara.

Kwa maneno rahisi watu wenye matatizo hayo walifanye papai kuwa rafiki yao wa karibu. Wanashauriwa kula papai asubuhi kabla ya kula chakula chochote, au watumie kijiko kidogo cha unga wa mbegu za papai baada ya kula chakula.

Tunda hili pia kusaidia kupona haraka kwa watu wenye matatizo ya vidonda (wounds), na pia ni msaada kwa watu wenye kansa ya ngozi. Watu hao wanashauriwa kutwanga majani ya mpapai na kupaka sehemu ya mwili iliyoathirika.

Post a Comment

 
Top