SURA YA TANO.
_____________
Kwa uchungu ambao ulikuwa umemshika Baba Jack alijikuta akielekea kule ilipo
Nyumba ya Mzee Shabani bila hata ya kushauriana na mtu yoyote, sijui nini
kilikuwa kimemsukuma kufanya vile maana hakuwa na mtu aliyethubutu kwenda
kwenye eneo lile tangia siku ile vijana walivyopotea kimaajabu na mahali pale palipo
geuka shimo la ajabu.
Muda tu ilisikika yowe la kuomba msaada yowe ambalo ilikuwa sauti ya Baba
Jack, hapo ilimtoa haraka ajabu Mzazu kuelekea sehemu ile huku baadhi ya
Wanakijiji wakiwa wanafatilia kuelekea mahali kule. Haikuchukua hata dakika tano,
Mzazu alikuwa amefika mahali pale na kuanza kazi.
Kazi ambayo kwa macho ya binaadamu wa kawaida hawa kuwa wakijua anafanya nini lakini walishangaa tu akidumbukia kwenye lile shimo wakati huo haikusika sauti ya Baba Jack baadala yake sauti za ajabu zilichukua nafasi kwenye masikio ya Wanakijiji walikuwa wakishuhudia lile zilidumu kama nusu saa mpaka pale Mzazu aliporejea na mwili wa Baba Jack ukiwa hauna uhai tena.
Kazi ambayo kwa macho ya binaadamu wa kawaida hawa kuwa wakijua anafanya nini lakini walishangaa tu akidumbukia kwenye lile shimo wakati huo haikusika sauti ya Baba Jack baadala yake sauti za ajabu zilichukua nafasi kwenye masikio ya Wanakijiji walikuwa wakishuhudia lile zilidumu kama nusu saa mpaka pale Mzazu aliporejea na mwili wa Baba Jack ukiwa hauna uhai tena.
Jambo ambalo liliwaliza sana Wanakijiji walikuwa sehemu ile nakuongeza
machungu ambayo kiasi fulani yalileta matumaini ya kijiji chao Maana Mzazu
aliwahakikishia Mzee Shabani amekimbia baada ya kumjeruhi vibaya na hata weza
kurejea mahali pale maana alishahamisha familia yake eneo lile na kuamia sehemu
nyingine ila alikuwa akileta fujo tu.
Maneno yale kidogo yaliwapa matumaini Wanakijiji japo mwanzoni hawakuwa na
imani na yale maneno lakini baada ya siku kadhaa tangia kufanyikwa kwa maziko
ya baadhi ya Wanakijiji waliopoteza maisha kutokana na uchawi wa Mzee Shabani
ikiwemo Baba Jack, hali kweli ilitulia.
Uzuri Mzazu aliweka dawa kwa kuzuia Wachawi ndani ya kijiji kweli ilionekana
kufanya kazi haswa maana ilipita wiki ikapita, mwezi ukapiata mwaka wa kwanza
na miaka mingine ikafata haikutokea tena kero ya jambo lile. Maisha ya wanakiji
cha Tangeni yakarudi kama zamani. Amani ikiwa imetawala kwa kiasi kikubwa huku
kila mwaka ikifanyika kumbukumbu ya kuwaenzi watu walipotea katika jambo lile
___________
Taswira ya Mama yangu kabisa niliweza kuiyona, taswira ambayo iliwafanya
wale wachawi wakiongozwa na Mzee shabani wakipotea eneo lile haraka. Niliona
mwili wangu ukiwa mwepesi kabla ya taswira ya Mama yangu kuanza kuzungumza na
mimi maneno ambayo yalikuwa yakielezea mambo yalikuwa yametokea kwenye kijiji
walichukuwa wakiishi ndani ya kijiji cha Tangeni miaka mitatu nyuma kabla ya
vifo vyao yeye na Baba, alizungumza kwa muda huku nikiwa namsikiliza vyema.
Kabla ya kupotea eneo lile na mimi macho yangu kufumbua kutoka kwenye usingizi
ule wa kulazimishwa.
Kufumbua kule kuliendana na mihemo isiyo kuwa na idadi wakati huo nilisikia
sauti ya jogoo iliyonifanya nijue muda si mrefu kungeweza kukucha na kunitoa
kwenye karaha ile ambayo nilikuwa nikipata kwenye usiku ule.
Nilifikiria sana hali ile, nikayakumbuka maneno ya Mjomba kuhusu kuwa mbali
na Mtoto wa Mzee Shabani ambaye mimi nilikuwa nimeshaanzisha uhusiano nae. Siku
ile aliponiona punde tu aliponikuta nimesimama nae maeneo ya kisimani. Mjomba
alinisema sana kuhusu binti Yule huku akinionya dhahiri kuwa Baba yake binti
yule si mtu mzuri kabisa.
Maneno ya Mjomba yalijurudia ndani ya kichwa changu moja kwa moja
nikihusinisha na tukio lilinitokea wazi nikaona ile haikuwa ndoto yale yote
yalikuwa yametokea usingizi ilikuwa kweli kabisa. Kweli ambayo sasa ilinipa
mawazo mengi huku nikiwa nimeshikwa uchungu dhidi ya Mzee yule. Kwa upendo
wazazi wangu sikudhani kama ipo siku nitaweza kuishi katika Dunia bila ya wao
jambo ambalo mwazoni linipa shida sana, chanzo cha vifo vyao ndio ilikuwa
ikinipa tabu sana nilikuwa natamani niweze kugundua mhusika wa vifo vile.
Sikuweza kulala tena mawazo mengi yalikuwa ya kinitawala juu ya lile na
niwazeje kuwa na mahusiano na binti ambaye Baba yake ndio mhusika wa vifo vya
ndugu zangu pomoja na wazazi wangu jambo ambalo sasa lilikuwa likiniumiza mno
akili ya kuachana na Mwajabu sasa ilikuwa imenitawala na vita dhidi ya Baba
yake ndio ilikuwa ikifata, sipo tayari kuona akiishi kwenye macho yangu
nilijisemea mwenyewe.
Muda nao haukuwa nyuma, ulienda mno na hatimaye kigiza kilianza kupotea huku
visauti tu ndege vikiwa tawala kwenye masikio yangu. Mwanzoni nilikuwa
nikipenda sana sauti za ndege haswa ndege aina ya kibinwe. Maana kucha asabuhi
ya siku nyingine ilikuwa lazima nisikie sauti yake kwenye ngome za masikio
yangu, lakini siku hiyo ilikuwa tofauti sana nilihisi ikichoma choma ngome za
masikio yangu na kuacha maumivu makali mno.
Nilitoka ndani kwangu na kwenda kuoga kabla ya kurejea tena na kujitupa
kitandani na usingizi hata ulipotokea tena maana nilikuja kushituka kijua
kinaanza kuwaka hivyo kuamka tu pale kitandani kulinifanya nitoke nje nikiwa na
wazo moja la kwenda kumwona moja ya marafiki zangu ilikuzungumza nae juu ya
jambo lile.
Nilitumia dakika chache na kuelekea kule haraka na uzuri nilimkuata na
kuanza kuongea naye juu ya ile ndoto lakini hakuonesha kushituka juu ya lile
zaidi ya kunimbia kuwa ile haikuwa ndoto ni kweli kabisa maana habari za kijiji
cha Tangeni alikuwa akizifahamu vyema na kuhusu habari za yule mzee alishawai
kuzisikia kutoka kwa Mzee wake kuwa si mtu mzuri kabisa. Hivyo ndoto yangu
ilikuwa si uongo kabisa yale niliyoyaona ni kweli kabisa namna alivyokuwa
akiniambia maneno yale yaliongeza chuki dhidi ya Mzee Shabani.
Lakini suala la kupambana na uchawi wa Mzee yule si suala dogo kabisa hivyo
iwe na subira tu nisikurupuke cha kufanya tu niwe mbali na mtoto wake .
Kiukweli hata Yona asingeniambia nikae mbali na yule binti nisingethubutu tena
kuwa karibu nae kabisa. Maana nilikumbuka kabisa lile lilitokea wakati
alipokuwa nae Nyumbani kuanzia ujio wake na hata alivyoondoka wazi ilinifanya
kuamini kuwa ni kweli kabisa kile akisemacho rafiki yangu Yona.
Maongezi yalikuwa mengi sana mpaka chakula cha mchana niliamua kula pale
kabla sijarudi nyumbani na kukutana na ujio wa Mwajabu ambao macho yangu hayakuwa
yakifurahia ujio ule kama mwanzoni ni wazi Mwajabu aliliona lile kwenye mboni
za macho yangu.
Nilimwomba aondoke eneo lile kabla sijamfanya kitu kibaya, maneno ambayo
yalimwingia vizuri Mwajabu wakati huo niliendelea kubwabwaja juu ya mambo
mabaya ya Mzee wake. Niliendelea kubwabwaja sana Mwajabu akiwa ananitazama tu
huku akiwa anachakufanya, niliongea mpaka nilijihisi kuishiwa pumzi ya kuongea
kile na hasira zangu kuanza kupungua. Hapo Mwajabu ndipo alipopata fursa ya
kuzungumza nami maneno ambayo yalinifanya niamini kiasi gani Mwajabu alikuwa
amejitolea maisha yake kwajili yangu japokuwa Mzee shabani alikuwa ni Baba yake
lakini vitendo vyake vya kishirikina vimekuwa vikimumiza.
Mbaya zaidi Mzee shabani aliweza kumua Mama yake kutokana tu na uchawi wake.
Kitendo ambacho hata yeye kinamuama sana na mbaya zaidi anataka kumwozesha kwa
mwanaume mwenye mambo ya kichwawi. Maneno ya Mwajabu yalisikia vyema kwenye
masikio yangu wakati huo nikijikuta machozi yananitoka.
Mwajabu alijisogeza taratibu mahali nilipo nakunikumbatia huku kwa dakika
kadhaa kabla ya kunichukua kuelekea ndani moja kwa moja kwenye kitanda
nilijikuta tunaangukia sehemu ile huku Mwajabu akinipapasa.
Kunipapasa kule nilishangaa tu tunafanya mapenzi na Mwajabu kwa mara nyingi
mara hii akiwa tofauti sana maana na mimi nilikuwa nimeshaanza kujua mchezo ule
hivyo nilijikuta nikishiriki tendo lile kikamilifu tofauti hata ilivyokuwa
mwanzoni. Tendo lile lilidumu kama masaa mawili kabla ya wote kujikuta tuiwa
hoi kutokana na jambo lile.
Maongezi yalichukua nafasi yake kabla ya kusikia kishindo cha ajabu nje kwa
namna ya kishindo kile kilitufanya kutoka ndani na kwenda nje. Ajabu tulikutana
na damu tu na shimo dogo eneo lile la nje ya nyumba yangu ilinifanya nishangae
kwa upande wangu lakini Mwajabu hata akushitushwa, zaidi ya kusema sasa utakuwa
mwisho wa Mzee Shabani. Sikumwelewa kwa nini Mwajabu alikuwa akiyanena yale.
Niliona sasa hali inaweza kuwa mbaya kwa upande wangu lakini Mwajabu
aliniambia Mama yake kabla ya kufa alijua wazi kuwa Mzee angemuua hivyo
aliniambia kuwa siku na dhama za mwisho za Baba zitakavyo kuwa hivyo, ile
ilikuwa dalili tosha wa mwisho wake. Aliongea Mwajabu huku akiwa hana hata
hofu.
Kweli kama alivyokuwa akinena baada ya siku ya pili kutokea lile Mzee
shabani aliagaa Dunia kwa ugonjwa hata ulikuwa haujulikani lakini kwenye
mazishi yake mambo ya ajabu yalijitokeza maana mipaka ililia usiku kucha na
hata baada ya maziko yake hali ilikuwa vile wakati huo Mwajabu hakuona haja ya
kukaa pale aliamia kwangu moja kwa moja jambo ambalo lilitafsirwa vibaya
mwanzoni na marafiki zangu haswa Yona na baadhi ya Wanakijiji.
Lakini kutokana na ndoto nilizokuwa nikiota juu ya lile haswa kutokea na
Mama kama ilivyokuwa mara ya kwanza walionesha kukubaliana na lile na kunipatia
Baraka ya kuishi naye na Mwajabu. Niliamua kuoa kabisa na baada ya maneno
maneno niliamua kuhama kabisa na kijiji kile na kuamia sehemu nyingine na
kuanza maisha ambayo haikuchukua muda Mwajabu alifanikiwa kunipatia mtoto wa
kike hali iliyongeza furaha tele ndani ya maisha yangu sikuwa na kinyongo nae
na yeye kabisa huku nikiamini lile lilikuwa chaguo sahihi sana kwangu.
MWISHO
HAKIKA ILIKUWA MTOTO WA MCHAWI WA KIJIJI. NAAM!, NAOMBA NIWASHUKURU WOTE
WALIOFANIKISHA KAZI HII KUFIKIA WEWE MSOMAJI. NA WEWE KUSOMA KAZI HII NAJUA
MWISHO WA KAZI HII NDIO MWANZO MZURI WA KAZI NYINGINE NDANI YA STORY ZA YONA
FUNDI. KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI KUPITIA NAMBA ZIFATAZO 0675278759.
RIWAYA MPYA MZURI NA YA KUSISIMUA INAPATIKANA HADI KWA MFUMO WA AUDIO IPO TAYARI
Post a Comment