Wanajeshi wa Sudan Kusini waliokuwa
wenye njaa wameiba chakula kutoka kwa mfanyibaishara mmoja katika moja
ya masoko makuu kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Juba.
Wakati
mfanyibiashara huyo katika soko la Konyo Konyo aliwataka wanajeshi hao
walipie chakula hicho, walimjibu na kumuambia aende kwa Rais Salva Kiir
kudai pesa zake kwa sababu hawajalipwa mishara kwa miezi kadha.
Wafanyibiashara wengine walifunga maduka yao ili wanajeshi hao wasije nao wakawaibie.
BBC
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.