SOMA HII ; Njia 14 za kuondoa tatizo la kuwahi kufika kileleni
Kuna sababu nyingi zinazoweza kupelekea kupotea kwa nywele kama vile:
a)Sababu za kimazingira,
b)Kuzeeka,
c)Msongo wa mawazo (stress),
d)Kuvuta sigara kupita kiasi,
e)Lishe duni,
f)Homoni kutokuwa sawa,
g) Kurithi
h) Maambukizi kwenye ngozi ya kichwa
i)Matumizi yasiyo sahihi ya vipodozi vya nywele
j)Baadhi ya dawa za hospitali
k)Matatizo katika kinga ya mwili
l)Upungufu wa madini chuma
m)Na magonjwa mengine sugu
Ni jambo la kawaida kupotea nywele 50 mpaka 100 kwa siku lakini unapoanza kupoteza zaidi ya hapo kwa siku ni muda muafaka kwako kuchukua hatua kurudishia kiasi hicho cha nywele kinachopotea.
Leo nimekuletea hapa orodha ya dawa za asili 6 zinazoweza kuotesha na kuzipa afya upya nywele zako ambazo zimeanza kupotea na hivyo kuondoa huo upara bila gharama sana.
Uvumilivu unahitajika zaidi kwani ni tiba inayochukua muda mrefu kwa kawaida.
1. Uwatu
- Loweka katika maji kikombe kimoja cha mbegu za uwatu kwa usiku mmoja.
- IAsubuhi yake zisage upate kama gundi (paste).
- Pakaa hiyo gundi kwenye nywele zako na ujifunike na kofia ya kuogea kwa dakika 40.
- Fanya zoezi hili kila siku asubuhi kwa mwezi mmoja hivi.
Kitunguu maji huua bakteria wabaya kitendo kinachosadia kuua vimelea na wadudu wa magonjwa kwenye ngozi ya kichwa vitu ambavyo huweza kupelekea kupotea kwa nywele (upara).
Utafiti unaonyesha juisi ya kitunguu kuwa na uwezo mkubwa kutibu tatizo la kupotea kwa nywele kwa mjibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la Dermatology mwaka 2002 huku wakitoa majibu ya zaidi ya asilimia 74 ya washiriki wa utafiti huo kupata kurejeshewa nywele zao zilizokuwa zimeanza kupotea.
- Chukua juisi ya kitunguu maji kimoja na uipake moja kwa moja sehemu ambayo nywele zimeanza kupotea na uache kwa dakika 30 kisha jioshe baadaye na shampoo
- Mau changanya pamoja vijiko vikubwa vitatu vya chakula vya juisi ya kitunguu maji na vijiko vikubwa vingine vya jeli ya aloe vera. Unaweza pia kuongeza kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya zeituni na upake mchanganyiko huo kichwani sehemu ambayo nywele zimeanza kutoota. Acha kwa dakika 30 ujisafishe na shampoo baadaye.
3. Aloe Vera (mshubiri)
Chukua majimaji ya mshubiri fresh (jeli) na upakae kichwani sehemu ambayo nywele zinanyonyoka na uache kwa masaa kadhaa na ujisafishe na maji ya uvuguvugu. Fanya zoezi hili mara 3 mpaka 4 kwa wiki. Unaweza pia kunywa juisi fresh ya mshubiri kila siku asubuhi tumbo likiwa tupu kuongeza ufanisi wa ukuwaji wa nywele zako na afya yako kwa ujumla.
4. Juisi ya Kiazisukari. (Beetroot)
- Mara kwa mara kunywa juisi fresh ya kiazisukari pia juisi ya karoti fresh ili kuongeza afya ya nywele zako.
- Au twanga majani kadhaa ya kiazisukari na uyachemshe kwenye moto kidogo ukichanganya na hina na upake mchanganyiko huo kichwani sehemu ambayo nywele hazioti. Acha kwa dakika 15 na ujisafishe na maji safi. Rudia tendo hili mara kadhaa katika wiki.
- Tengeneza tui lako zito kidogo ukitumia nazi, ili kupata tui zito na jingi nakushauri kisha kukuna nazi yako iweke kwenye blenda na maji kidogo kwa mbali kisha iblendi kwa dakika kadhaa ndipo ukamuwe upate tui zito kabisa na jingi.
- Mimina tui hilo kwenye sufuria na uweke kwenye moto kama dakika 3 au 4 hivi kisha ipua
- Once Subiri tui hilo lipowe na mwisho pakaa kichwani kichwa chote au sehemu ambayo nywele zimepotea na uache hivyo kama dakika 20 kisha safisha kichwa na shampoo ya aloe vera (mshubiri).
- Kufanya dawa iwe na nguvu zaidi unaweza kuongeza ndani ya tui la nazi nusu kijiko cha achai cha unga wa pilipili manga nyeusi na kiasi hicho hicho cha unga wa mbegu za uwatu.
Ingawa haieleweki ni kwa namna gani mafuta haya yanakuza nywele lakini wanasayansi wanaamini haya yanaweza kuwa ni matokeo uwezo wake mkubwa wa kuondoa sumu na protini nyingi ndani yake. Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya nywele yenyewe ni meusi kabisa kabisa na huwa mazito kidogo.
Matumizi: Sugulia kipande cha limao fresh eneo ambalo nywele zimenyonyoka na kisha pakaa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya habbat soda ya nywele na uache kama dakika 15 hadi 20, unaweza kuacha hivyo hivyo au ujisafishe na maji safi, unaweza kufanya kutwa mara 1 au 2 kwa mwezi mmoja hadi miwili.
Ikiwa utahitaji mojawapo ya hizi dawa Tuwasiliane, WhatsApp +255719136173
Kama una swali unahitaji ushauri zaidi niachie ujumbe hapo kwenye comment ni faraja kwangu kuona nimekujibu vizuri
Wao nimependulivyo elezea hayo mafuta ya nywele ni bei gan
ReplyDelete