Raia wa Los Angeles
ambao ndio majirani wa eneo la kuigiza filamu maarufu 'Hollywood'
waliamka mwaka mpya na kuona kwamba ubao wa ishara ya eneo hilo maarufu
umebadilishwa na kuwa 'Hollyweed'.
Vyombo vya habari katika eneo
hilo vimeripoti kwamba maafisa wanalichukulia swala hilo kuwa dogo na
kwamba wanaendelea na uchunguzi.Ishara hiyo ilioko katika mlima Lee ina herufi zenye urefu wa futi 45.
Wapiga kura mjini California waliidhinisha sheria ya kuhalalisha bangi katika kura iliofanyika wakati mmoja na uchaguzi wa Marekani mnamo tarehe 8 Novemba.
Mzaha huo hatahivyo haujaharibu herufi za ishara hiyo kwa kuwa herufi 'O' zilifanywa na kuwa 'E.'
Gazeti la Los Angeles Times limeripoti kwamba mtu mmoja alirekodiwa akipanda katika ishara hiyo ili kubadilisha herufi hizo.
Mzaha kama huo ulifanyika mnamo mwaka 1976 ili kulegeza sheria dhidi ya bangi.
Post a Comment