0
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila OdingaJanuary 30, 2018 aliapishwa kuwa ‘rais wa wananchi’ nchini humo baada ya kusema hatambui ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa marudio uliofanyika October 2017.
Raila Odinga sio wa kwanza kujiapisha katika bara la Afrika wapo viongozi wengine ambao nao walijiapisha ikiwa kuna Rais madarakani. Nimekusogezea list ya viongozi wanne waliojiapisha.
Etienne Tshisekedi alikuwa kiongozi mkuu wa upinzani, wakati wa utawala wa Rais Mobutu Sese Seko Zaire, na baadaye Laurent Kabila Joseph Kabila wa DRC
November 2011, Tshisekedi aligombea Urais akichuana na Laurent Kabila, kisha aliamua kujiandalia kiapo mwenyewe na kuapishwa nyumbani kwake na mkuu wa watumishi wake Albert Moleka. Baadaye aliwekwa katika kizuizi cha nyumbani.
Nchini Nigeria pia tukio kama hili lishawahi kutokea, Moshood Abiola alijitangaza mwenyewe kuwa Rais kipindi ambacho Rais Sani Abacha alipokuwa madarakani.
Alikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini na kufungwa jela kwa miaka minne hadi ilipofika mwaka 1995, alifariki muda mfupi baada ya kunywa chai akiwa katika mkutano nchini Marekani
Mwaka 2016 Gabon, kiongozi wa upinzani Jean Ping alijitangaza mwenyewe kuwa Rais na kutoa wito kura kurudiwa kuhesabiwa kwa kura ambazo zilithibitisha kwamba Ali Bongo ameshinda.
Hata hivyo Dunia nzima ilijua kwamba Ping ndiye alikuwa rais wa nchi hiyo
Nchini Uganda Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye, ambaye ni mpinzani wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni, kupitia kanda ya video alionekana akifanya sherehe za kula kiapo mwaka 2016. Alikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.

Post a Comment

 
Top