Mkuu wa wilaya ya Liwale Mh Ephraim Mmbaga ambaye ndio mgeni rasmi
Shule ya sekondari ya Liwale high school imefanya mahafali ya
wanafunzi 148 kidato cha nne mahali yaliyofanyika katika ukumbi wa Malecela
uliopo shuleni hapo leo ambapo mgeni rasmi ni mkuu wa wilaya ya Liwale
mheshimiwa Ephraim Mmbaga.
Liwale high school ilianzishwa mwaka 1990 na kuanza kupokea
wanafunzi wa kidato cha tano mwaka 2008 na kuweza kufanyikiwa kufaulisha idadi
kubwa ya wanafunzi na kuweza kujiunga na
vyuo mbalimbali.
Mkuu wa shule Elly John
Moses hiyo akisoma risala mbele ya mgeni rasmi alisema wanafunzi
wanaohitimu ni 148 kati yao wavulana ni 74 na wasichana 74 na wanafunzi 12
wamekosa kuhitimu kutokana na sababu mbalimbali.
Moses aliyataja mafanyikio wameweza kuchimba visima viwili
vya kuhifadhia maji kwenye mabweni,kukalabati majengo,kutoa wanafunzi wa kidato
cha nne na sita wanaojiunga na vyuo mbalimbali pia alitoa changamoto
zinazoikumba shule ikiwemo uhaba
wa miundo mbinu ya majengo,upungufu wa watumishi,uhaba wa nyumba za walimu
kwani hivi sasa kuna nyumba za walimu 11 na idadi ya walimu na watumishi ni 33,ukosefu
wa usafi na ukosefu wa uzio eneo la shule hiyo.
Mmbaya ambaye katika hutuba yake kama mgeni rasmi
aliwapongeza wanafunzi wanaohitimu pia
aliwaomba wanafunzi hao wajitahidi kusoma ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani
na kuweza kutimiza malengo yaliyokuwa wenye tija kwao na kwa jamii.
Pia aliwasii na kuwaomba wananchi juu ya siku ya kupiga kura
kuwachagua wagombea wanaowaona wanafaa bila kulazimishwa na mtu yeyote ili
kuepuka mgawanyiko kwani kuna maisha baada ya uchaguzi.
Post a Comment