Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano aliyemaliza muda wake, Job Ndugai.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano
aliyemaliza muda wake, Job Ndugai, amesema timu zilizoundwa na Bunge
kushughulikia vurugu za gesi zilizotokea mkoani Mtwara na mauji ya
Kiteto, zilishamaliza kazi na kuwasilisha ripoti za uchunguzi kwa
mamlaka husika.
Akizungumza na Nipashe , Ndugai alisema timu iliyoundwa na Bunge
kuchunguza mauaji yaliyotokea Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara,
iliongozwa na Askofu wa Kanisa la Mennonite, Amos Muhagachi.
Alisema timu hiyo ilifanya kazi kwa mwezi mmoja na walifanya utafiti uliohusu chimbuko la mauaji hayo pamoja na matatizo.
Ndugai alisema kuwa kuhusu timu iliyoundwa kuchunguza vurugu za
geni zilizotokea mkoani Mtwara, timu hiyo nayo ilishakamilisha kazi yake
na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda, lakini haikusomwa
bungeni na ilipelekwa moja kwa moja serikalini.
“Kimsingi timu zote hizo mbili zilizoundwa zilikamilisha kazi yake
na kuwasilisha taarifa zao bungeni na Bunge lilipeleka moja kwa moja
katika mamlaka husika,” alisema Ndugai.
Mwaka jana kulizuka mapigano baina ya wakulima na wafugaji yaliyosababisha vifo kadhaa. katika Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.
Kutokana na hali hiyo, serikali iliunda timu ya watu 10 kutoka kada
tofauti wakiwamo viongozi wa dini ambao walipewa jukumu la kufanya kazi
ya usuluhishi kwenye vijiji vyenye migogoro wakiongozwa na Askofu
Muhagachi.
Kadhalika, Mei 22, mwaka juzi, vurugu zilizotokea mkoani Mtwara,
Bunge la Jamhuri ya Tanzania liliamua kuunda timu ya wabunge 13
Ikiongozwa na Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage.
Kamati hiyo ilipewa jukumu la kuchunguza chanzo cha vurugu hizo,
kufuatilia hatua zilizochukuliwa na serikali kushughulikia mgogoro huo,
kukutana na wadau wa sakata hilo na kuchunguza mambo mengine yenye
uhusiano na mgogoro huo.
CHANZO: NIPASHE
Post a Comment