0
Mshambuliaji wa Liverpool Mario
Balotelli amewasili katika kilabu
ya AC Milan ili kufanyiwa ukaguzi
wa matibabu kabla ya kurudi
katika timu hiyo kwa mkopo wa
mwaka mmoja kilabu hiyo
imetangaza.
Baloteli amekubali kupunguziwa
mshahara ili kurudi Milan huku
Liverpool pia ikimlipa marupurupu
yake.
Mshambuliaji huyo wa Italy
mwenye umri wa miaka
25,huenda akacheza mechi yake
ya kwanza katika ligi ya Serie A
dhidi ya mahasimu wao Empoli
siku ya jumamaosi.
Aliifungia Liverpool bao moja
pekee baada ya kuhamia
Liverpool kutoka Milan kwa pauni
milioni 16 mnamo mwezi Agosti
mwaka 2014.
Aliwachwa nje katika mechi za
kirafiki za kikosi cha Liverpool
huko mashariki na Australia na
amekuwa akifanya mazoezi mbali
na kikosi cha kwanza.
Liverpool imewasajili Christian
Benteke,Roberto Firmino na
Danny Ings,huku Divock Origi
akiwasili.

Post a Comment

 
Top