0
Simba na Kakamega HomeBoyzHaki miliki ya pichaSPORTPESA
Mabingwa wa ligi ya Tanzania bara Simba wametinga fainali ya michuano ya Super Cup ya kampuni ya Sportspesa baada ya kuwacharaza Kakamega Homeboyz wa Kenya kwa mikwaju 5-4 ya penalti.
Simba walipata ushindi huo kwenye nusu fainali iliyochezewa uwanja wa Afraha, Nakuru.
Walifika nusu fainali baada ya kuwaondoa Kariobangi Sharks wa Kenya.
Klabu hiyo sasa itamsubiri mshindi wa nusu fainali kati ya mabingwa wa ligi Kenya Gor Mahia na Singida FC ya Tanzania kufahamu nani atakuwa mpinzani wao fainali.
Kwa sasa mechi inaendelea na Gor Mahia wanaongoza 1-0.
Bao hilo limefungwa na Meddie Kagere.
Singida FC walifika nusu fainali na kuwaondoa mahasimu wa jadi wa Gor Mahia AFC Leopards.
Kakamega HomeboyzHaki miliki ya pichaSPORTPESA
Kakamega Homeboyz ndio waliokuwa wamewatoa mashindanoni timu kongwe nchini Tanzania Yanga kwa kuipachika mabao 3-1 kwenye mechi ya ufunguzi.
Jumla ya dola 57,500 zitashindaniwa katika mashindano hayo.
Mshindi wa mashindano hayo atasafiri hadi England kutoana jasho na Everton katika uwanja wao wa Goodison Park mwezi wa saba.
Mashabiki wa Simba uwanjaniHaki miliki ya pichaSPORTPESA
Image captionMashabiki wa Simba uwanjani
Shabiki wa Kakamega HomeboyzHaki miliki ya pichaSPORTPESA
Image captionShabiki wa Kakamega Homeboyz
Bingwa mtetezi Gor Mahia ndiyo iliyocheza na Everton mwaka jana jijini Dar es Salaam ikapoteza kwa mabao 2-1, wafungaji wa Everton wakiwa ni mchezaji nyota wa zamani wa Manchester United Wayne Rooney na Kieran Dowell, naye Jacques Tuyisenge akaipa Gor Mahia bao lao moja.

Post a Comment

 
Top