Image captionMwandishi wa habari wa Ghana Anas Aremayew Anas akihojiwa na wanahabari kuhusu makala yake ya upelelezi yaliochukua miaka miwili
Takriban maafisa 100 wa kandanda katika eneo la Afrika Magharibi na Kenya walipatikana katika kamera wakipokea fedha katika operesheni kali.
Ni miongoni mwa upelelezi wa miaka miwili uliofanywa na mwandishi wa Ghana mwenye utata Anas Aremeyaw Anas. Kipindi cha BBC Africa Eye kimepata kanda za video za kipekee katika makala yao ya mwisho.
Katika kisa kimoja naibu refa kutoka Kenya anayeelekea Urusi kuchezesha dimba la dunia kutoka Kenya alikubali dola 600 kutoka kwa mtu aliyejifanya kuwa afisa wa shirikisho la soka la Ghana.
Fifa inasema kuwa refa huyo kwa Jina Aden Range Marwa , ambaye ni mmojawapo wa marefa walioteuliwa na Fifa kushiriki katika kombe la dunia nchini Urusi , hataelekea tena Urusi baada ya kupatikana akipokea zawadi ya $600.
Marwa alipewa fedha hizo na mwandishi mpelelezi aliyejifanya kuwa afisa mkuu wa timu moja kuu ya Ghana. Hatahivyo refa huyo amekana kufanya makosa yoyote.
Mwanachama wa baraza la Fifa nchini Ghana Kwesi Nyantakyi , ambaye ndiye afisa wa pili kwa uwezo katika soka ya Afrika , pia alipatikana na operesheni hiyo kali.
Alionekana akipokea $65,000 kutoka kwa mwandishi mpelelezi aliyejifanya kuwa mwekezaji katika soka ya Ghana.
Nyantakyi amekataa kutoa tamko lolote. Kwa jumla zaidi ya marefa 100 na maafisa wakuu walipatikana katika kamera wakichukua fedha kinyume na sheria za Fifa na GFA .
Makala hiyo iliofanywa na mwandishi aliyezua utata Anas Aremayaw Anas imezua maswali makali kuhusu hatma ya mchezo wa kandanda wenye ushabiki mkubwa barani Afrika.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionAliyekuwa beki wa zamani wa klabu ya Real Madrid fernando Hierro
Aliyekuwa beki wa Real Madrid Fernando ...Read more »
Haki miliki ya pichaSPORTPESA
Mabingwa wa ligi ya Tanzania bara Simba wametinga fainali ya michuano ya Super Cup ya kampuni ya Sportspesa baada ya ku...Read more »
Image captionAliyekuwa kocha wa Ufaransa na PSG Laurent Blanc
Chelsea inakaribia kumsajili aliyekuwa kocha wa Ufaransa na PSG Laurent Blanc kuchukua ...Read more »
Mwanamasumbwi wa Marekani Floyd Mayweather ametetea taji lake katika porodha ya Forbes ya wanamichezo wanaopata mapato ya juu zaidi duniani.
...Read more »
Mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 26, alikubali kujiunga na Real Madrid kabla ya Zinedine Zidane kujiuzulu kama kocha wa mabingwa hao...Read more »
Post a Comment
aprieztmkrdezign
218168578325095
Emoticon
Click to see the code! To insert emoticon you must added at least one space before the code.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.