Wanariadha wanane wa Cameroon hawaonekani katika makaazi yao katika michezo ya Jumuiya madola nchini Australia, maafisa wa timu hiyo wanasema.
Afisa wa habari Simon Molombe ameiambia BBC kwamba maafisa wanachukulia kama wanariadha hao wametoroka na kwamba wameripotiwa kwa maafisa wa polisi nchini humo.
Waenushaji vyuma vya uzito watatu na mabindia watano walionekana mara ya mwisho katika muda tofuati Jumatatu na Juamnne, alisema.
Cameroon imesema kundi la wanariadha hao wana viza halali za kudumu hadi Mei 15.
Olivier Matam Matam, Arcangeline Fouodji Sonkbou and Petit Minkoumba, wanaoinusha vyuma vya uzito na mabondia Christian Ndzie Tsoye, Simplice Fotsala, Arsene Fokou, Ulrich Yombo na Christelle Ndiang ndio waliotajwa kutoweka.
"Maafisa wamevunjwa moyo sana na kutoweka kwa wanariadha hawa - baadhi yao hata hawakushindana," Molombe amesema.
"Matumaini makubwa ni kwamba warudi na wasafiri kurudi nyumbani na wenzao."
Serikali ya Australia imewaonya wanariadha dhidi ya kukaa zaidi ya muda walioruhusiwa.
Shirikisho la michezo hiyo ya Jumuiya ya madola limesema litaikagua hali hiyo, lakini limeongeza kwamba wanariadha wana "haki ya kusafiri kwa uhuru" kwa viza walizo nazo.
Polisi ya Australia imejulishwa kuhusu hali inavyoendelea, kwa mujibu wa Kate Jones, waziri katika jimbo la Queensland.
Post a Comment