0

Kuna baadhi ya watu huona ndevu kama uchafu na hazina maana yoyote. Amakweli!, ‘usilolijua ni sawa na usiku wa giza’.

Kwa mujibu wa tafiti mbali mbali duniani za wataalam ukiwemo utafiti ulliofanya na Dk. Freedman, mtaalam wa maswala ya Saikolojia ya Kijamii ama kwa lugha ya kitaalam ‘Social psychology ‘.

Mbali ya kuwa ndevu humfanya mwanaume avutie zaidi kwa mwanamke, hizi ni faida za kiafya za mwanaume kufuga ndevu;-

1. Ndevu hulinda uso dhidi ya kemikali hatari pamoja na hewa chafu ambazo kimsingi husababisha uharibu wa chembe chembe hai za mwanadamu. Pia husaidia ngozi ya usoisizeeke haraka, isiwe na mikunjo na kuifanya ngozi kuwa yenye kuvutia.

2. Ndevu huifunika ngozi ya uso, ambapo hulinda tezi za mafuta zishambuliwe na bakteria hivyo humfanya mtu asiwe na chunusi.

3. Kuweka uso wako joto na kulinda kidevu chako kutokana na hatari.

4. Ni kuzuia ugonjwa wa koo na ufizi.

5. Matatizo mengi ya mfumo wa upumuaji huzuiwa kwa kufuga ndevu.

Sanjari na hayo;

6. Ndevu ni utambulisho wa mtu kuwa ni wa heshima kwa mwanamke.

7. Utafiti unasema kuwa kadri ndevu zinavyo kuwa nyingi ndivyo mtu anavyozidi kuwa na hekima.

Je, kwa ujumla mwanaume hutumia muda gani katika maisha yake yote kunyoa ndevu?


Usipate tabuya kuanza kuhesabuDk Herbert mescon, kutoka Chuo Kikuu cha Boston, alifanya utafiti kutoa jibu la swali hili.

Dk. Mescon alihesabu kwamba kama kijana ataanza kunyoa ndevu akiwa na umri wa miaka 15, hivyo kama ataishi miaka 55 huku akiwa ananyoa ndevu katika maisha yake, basi mtu huyo anaweza kutumia masaa 3350 kunyoa ndevu katika maisha yake yote, ambapo ni sawa na siku 139.

Hii ni ajabu!, utumie muda wako wote huo kwenye maisha yako kwa ajili ya jambo moja tu, ati kunyoa ndevu!. Hivi ungeweza kuingiza kiasi gani cha pesa kama ungetumia muda wako kufanya shughuli nyingine? Kumbuka waswahili wana usemi usemao ‘Muda mali’. Usisahau afya yako pia.

Je upo tayari kufuga ndevu na ukanufaika na hizo faida 7 ?

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top