0
Kocha wa klabu ya Nice ya Ufaransa Lucien FavreHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKocha wa klabu ya Nice ya Ufaransa Lucien Favre
Kocha wa klabu ya Nice ya Ufaransa Lucien Favre anatajwa kuwa kwenye orodha ya walimu wanaotajwa kuwa huenda wakarithi nafasi ya kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ifikapo mwishoni mwa msimu huu wa ligi, gazeti la L'Equipe la Ufaransa limeripoti.
Kocha wa Gunners Arsene Wenger ana imani kuwa "kiungo wa Wales mwenye umri wa miaka 27 Aaron Ramsey ambaye mwishoni mwa msimu ujao atakuwa amemaliza mkataba wake, atatia saini mkataba wa muda mredu katika klabu yake ya Emirates. (Mail)
Kocha wa klabu ya Tottenham Mauricio Pochettino anasema mshahara wa paundi milioni 6.01 anaopokea Daniel Levy ambao ni sawa na paundi 115,000 kwa wiki aliokuwa anapata mwaka uliopita "sio tatizo Kwa wachezaji", licha ya mpango wa klabu kujaribu kupunguza mshahara wa kikosi chake. (Times)
Kocha wa klabu ya Chelsea Antonio Conte anasema "anahuzunika" Kwa namna timu yake imefanya katika kujaribu kutetea taji la ligi Kuu msimu huu lakini akakanusha uvumi kuwa ataachana na klabu hiyo akiongeza kuwa lengo lake ni "kubakia" na kuendeleza kazi yake kwenye klabu". (Guardian)
Kiungo wa klabu ya Manchester City Kevin de BruyneHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKiungo wa klabu ya Manchester City Kevin de Bruyne
Kiungo wa klabu ya Manchester City Kevin de Bruyne mwenye umri wa miaka 26, anasema "sauti mara zote imekuwa juu" wakati wanacheza muziki wao na sio "kumkejeli yeyote". Kocha wa Manchester United Jose Mourinho alilalamika kuhusu sauti ya juu ya muziki kutoka kwenye vyuma vyao vya kubadilishia nguo wakati walipoifunga timu yake mwanzoni mwa msimu. (Mirror).
Mshambuliaji wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan, 29, anaweza kuwa nje ya uwanja msimu mzima baada ya kupata jeraha la goti wakati timu yake ilipocheza na CSKA Moscow siku ya Alhamisi. (Telegraph).
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameanza mchakato wa kupata saini beki wa kushoto wa klabu ya Monaco, Mfaransa Djibril Sidibe, 25. (Le10Sport )
Mchezaji wa klabu ya Real Madrid Gareth BaleHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMchezaji wa klabu ya Real Madrid Gareth Bale
Mchezaji wa klabu ya Real Madrid Gareth Bale, 28, amesema hana mpango wa kuondoka kwenye klabu yake msimu huu licha ya mshambuliaji huyo wa Wales kuachwa nje kwenye mechi za hivi karibuni. (AS)
Klabu ya Liverpool imeonesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Monaco Christian Koffi, raia huyu wa Ivory Coast mkataba wake unafikia tamati katikati ya msimu ujao. (Mail)
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane na kocha wa Ufaransa Didier Deschamps wamo kwenye orodha ya kuruthi nafasi ya kocha wa Juventus Massimiliano Allegri ikiwa ataenda kujiunga na klabu ya Chelsea. Zinedine na Deschamps wote waliwahi kucheza nafasi ya kiungo kwenye klabu ya Juventus. (London Evening Standard)
Klabu ya Inter Milani imeipiku klabu ya Arsenal katika mbio za kupata saini ya mlinda mlango wa klabu ya Zorya Luhansk, Andriy Lunin na kukubali kulipa paundi milioni 5.5 Kwa Kopa huyo mwenye umri wa miaka 19 raia wa Ukraine. (Gazzetta dello Sport la Italia)
Klabu ya Arsenal imeripotiwa kuwa inamfuatilia kiungo mwenye umri wa miaka 18 anayekipiga na klabu ya Benfica, Joao Felix, ambaye kwenye mkataba wake kuna kipengele cha paundi milioni 25 kuuvunja lakini inawezekana akagharimu paundi milioni 35. (O Jogo, kupitia Mirror).
Andre GrayHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAndre Gray
Kocha wa klabu ya Watford Javi Gracia amesema mshambuliaji wake Andre Gray ni "mchezaji mzuri" lakini akakataa kutoa hakikisho lolote kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ikiwa atasalia klabuni hapo. (Hertfordshire Mercury)
Klabu za Crystal Palace, Aston Villa na Malaga wako kwenye mbio za kumuwania kiungo wa kimataifa wa Australia Massimo Luongo,25 kutoka klabu ya QPR. (SBS)
Kocha Stevenage amemuacha beki wake Ben Wilmot mwenye umri wa miaka 18 kutoka kwenye orodha ya kikosi chake kitakachokaikabili klabu ya Newport siku ya Jumamosi wakati huu kukiwa na uwezekano mkubwa wa kuuzwa Kwa klabu ya Arsenal au Tottenham.(Sun)
Kocha wa klabu wa Newcastle Rafael Benitez amemuunga mkono kiungo wake Jonjo Shelvey kuwa atapata nafasi kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya England kitakachoshiriki fainali za kombe la dunia, akisema kiungo wake "ni tofauti na wachezaji wengine na ana uwezo wa kutoa mchango mkubwa". (Guardian)

Post a Comment

 
Top