0
Utetezi uliotolewa na mashaidi haukuaminikaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionUtetezi uliotolewa na mashaidi haukuaminika
Muigizaji nyota wa filamu za Bollywood Salman Khan,amepewa dhamana siku mbili baada ya mahakama kumpa hukumu ya miaka mitano jela kwa kuua aina mojawepo ya swala ambao ni adimu kupatikana duniani mwaka 1988.
Mahakama hiyo iliyoko Jodhpur ilimpa hukumu ya miaka mitano jela pamoja na kumtoza faini ya rupia 10,000 ($154; £109) kwa kosa hilo.Lakini leo mahakama imepokea dhamana yake.
Mahakama ilimuhukumu Khan mwenye umri wa miaka 52,aliuwa swala wawili ambao walikuwa kwenye hifadhi ya Rajasthan wakati akitengeneza filamu yake.
Kundi kubwa la watu lilikusanyika nje ya gereza hilo wakiwa wanacheza ,wakipiga kelele na kuimba mara baada ya kupata matokeo ya hukumu ya muigizaji huyo.
Mwandishi wa BBC,nchini India anasema maoni ya watu hao yalikuwa yanatofautiana juu ya muigizaji huyo kama ni sawa apate dhamana au adhabu kali.
Mashabiki wake wakionyesha upendo nje ya jela alilofungwa KhanHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMashabiki wake wakionyesha upendo nje ya jela alilofungwa Khan
Waigizaji wengine wanne ambao walishtakiwa naye baada ya kukamatwa wakiigiza naye filamu hiyo walikutwa hawana hatia.
Khan ambaye alifungwa jela kwa siku mbili ana mpango wa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo kwa mahakama ya juu.

Nini chanzo cha kesi ya Khan?

Hii ni kesi ya nne iliyowasilishwa dhidi ya mwigizaji huyo inayohusiana na uwindaji haramu wa wanyama wakati walipokuwa wakiigiza filamu ya Hum Saath Hain mwaka 1988.
Hata hivyo filamu iliyosababisha Salman Khan kuingia hatiani imepata umaarufu mkubwa nchini India ,mijini na vijijini.
Khan amekuwa akipata heshima kubwa nchini mwake kutokana na kazi yake.
Ingawa sasa hukumu hii inaweza kupoteza thamani ya umaarufu wake na hata kuharibu kazi yake.

Post a Comment

 
Top