Mahakama nchini Kenya imempa msichana wa shule dola 40,000 baada wa kuvuliwa nguo na polisi waliokuwa wakitafuta madawa ya kulevya katika kisa kilichotokea mwaka 2015.
Picha za msichana huyo zilidaiwa kuchukuliwa na polisi na kisha kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Mahakama ilisema kuwa haki za msicha huyo wa miaka 18 wa shule ya upili zilikiukwa.
Gazeti la Standard linasema kuwa msichana huyo alipiowa picha akiwa nusu uchi na picha hizo kufuja kwa mitandao ya kijamii.
Msichana huyo kisha akapeleka kesi mahakamani akisaidiwa na shirika moja la kupigania haki za watoto akisema kuwa picha hizo zilimuathiri ambapo alitaka alipwe dola 70,000.
Gazeti la Standard lilisema kuwa msichana huyo alikuwa miongoni mwa wanafunzi wengine 44 waliakamawa katika kituo kimoja cha biashara kaunti ya Nyeri.
Post a Comment