0


Happy Sea OtterHaki miliki ya pichaPENNY PALMER/ BARCROFT IMAGES

Huu hapa ni mkusanyiko wa picha za kuchekesha na kusisimua za wanyama zilizopigwa mwaka huu, miongoni mwa picha hizi ikiwa moja ya dubu wanaoonekana kukoleza uhusiano wao pamoja na nyingine ya sili.
Picha hizi ziliteuliwa kushindania tuzo za picha za ucheshi za wanyama mwaka huu, katika vitengo vitano.
Jumla ya picha 3,500 ziliwasilishwa kwa mashindano hayo.
Shindano hili huandaliwa kuchangisha pesa na kusaidia shirika la kutetea uhifadhi wa wanyama la Wakfu wa Born Free.

OwlsHaki miliki ya pichaTIBOR KERCZ/ BARCROFT IMAGES
Image captionPicha hii ya Tibor Kercz ilipewa kichwa 'Nisaidie'

Mshindi wa jumla Tibor Kercz kwa picha hii yake ya bundi anayeonekana kuhitaji usaidizi kujishikilia vyema kwenye tawi mti alitunukiwa kikombe ambacho kilitengenezwa na wanaume na wanawake wenye ulemavu kutoka Tanzania.
Kadhalika, alipewa vifaa zaidi vya kupigia picha.
Alishinda pia tuzo kwenye kitengo cha picha ya kuvutia zaidi ya mtandaoni pamoja na kujishindia safari ya kwenda mbugani Kenya.
Kabla ya picha hii ya Andrea Zampatti kushinda kitengo cha picha za ardhini, picha hii yake ya panya anayeonekana kuangua kicheko ilisambazwa sana mitandao ya kijamii mapema mwaka huu.

DormouseHaki miliki ya pichaANDREA ZAMPATTI /BARCROFT IMAGES
Image captionRaha mustarehe!

Na ingawa bahari ni kubwa, picha hii iliyoshinda kitengo cha picha za chini ya bahari inaonesha viumbe wanaweza bado kukaribiana sana.

Turtle and fishHaki miliki ya pichaTROY MAYNE/ BARCROFT IMAGES
Image captionPicha hii ilipewa kichwa 'kofi'

Kitengo cha picha za angani, picha hii ya njiwa mmoja wao akionekana kufuata njia ya moshi wa ndege, iliyopigwa na John Threlfal Preston, Lancashire ndiyo iliyoshinda.

Birds.Haki miliki ya pichaJOHN THRELFAL/ BARCROFT MEDIA

Hapa chini ni baadhi ya picha nyingine zilizofanya vyema.

PenguinsHaki miliki ya pichaCARL HENRY/ BARCROFT IMAGES
Image captionTwende kanisani
RabbitHaki miliki ya pichaOLIVIER COLLE/ BARCROFT IMAGES
Image captionKunani?
Polar bearsHaki miliki ya pichaDAISY GILARDINI/ BARCROFT MEDIA
Image captionNibebe
WilderbeestHaki miliki ya pichaJEAN-JACQUES ALCALAY/ BARCROFT IMAGES
Polar bearsHaki miliki ya pichaBENCE MATE/ BARCROFT IMAGES
Image captionMapenzi tele
SealsHaki miliki ya pichaGEORGE CATHCART/ BARCROFT IMAGES
Image captionEti nini!?


Post a Comment

 
Top