0

Mkuu wa wilaya ya Liwale,mh.Sarah Chiwamba na Mshauri wa wa jeshi la akiba “Mgambo”  wa wilaya ya Liwale, Saidi Machunda (kushoto) akikagua gwaride (picha na Liwale Blog)









Esha Mnyupe akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa jeshi la akiba 
 Mshauri wa jeshi la akiba “Mgambo”  wa wilaya ya Liwale, Saidi Machunda akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi
 Kamanda wa polisi wilaya ya Liwale,Edward Malogo akizungumza jambo na wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba pamoja na wananchi

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale, ndugu Justin Monko akizumza jambo




Mkuu wa wilaya ya Liwale,mh.Sarah Chiwamba amefunga mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo” katika kijiji cha Kichonda kata ya Kichonda ambapo jumla ya wahitimu 65 ikiwa wanaume 55 na wanawake 10 wamefuzu mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa miezi minne.

Sherehe za kufunga mafunzo hayo zimefanyika leo alhamisi novemba 23,2017 katika viwanja vya shule ya msingi Kichonda wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Akizungumza katika sherehe hizo,Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kutumia vyema mafunzo waliyoyapata huku akiwaasa kufanya shughuli za maendeleo ili kujiinua kiuchumi.

Mh.Chiwamba alisema kuwa wahitimu hao watakuwa chachu ya mabadiliko kwa vijana wengine na kuwa walinzi wa amani katika maeneo wanayoishi, kushiriki katika shughuli za maendeleo na kujiepusha na matendo maovu.

Naye Mshauri wa wa jeshi la akiba “Mgambo”  wa wilaya ya Liwale, Saidi Machunda alisema washiriki wa mafunzo hayo mwaka huu wameweza kujifunza masomo mbalimbali kama vile kwata,urai,usomaji wa ramani,usalama wa raia,usalama wa Taifa,zimamoto,sheria za kijeshi.

Pia waliweza kujifunza mafunzo ya huduma ya kwanza,usafi wa mazingira,uhamasishaji na uchangiaji wa damu kwa hiari, ujasiliamali na kuzui na kupambana na rushwa.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wahitimu Esha Mnyupe alisema kuwa wanaomba ofisi ya mkuu wa wilaya pamoja na ofisi ya mshauri wa jeshi la akiba  kuharikisha vyeti pamoja na vitambusho na kusaidiwa kwenye suala la ajira.


Pia Bashiru Lijunga akiwa mmoja wa wahitimu alisema mafunzo waliyopatiwa yameweza kuwabadilisha kuwa raia wema na kufahamu utendaji wao wa kazi huku akitoa wito kwa vijana waliokosa kujiunga na jeshi la akiba kuweza kujiunga ili kuweza kupata kozi ya mafunzo mbalimbali.

Post a Comment

 
Top