0
 
Azam wakishangilia bao
Sasa hakuna ubishi tena. Baada ya kuvuliwa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu ya Azam FC hatimaye imekata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa Yanga SC katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo ilikuwa ni kukamilisha ratiba tu kwa Yanga, ambao wamekuwa mabingwa wiki moja iliyopita. Lakini kwa upande mwingine,ushindi huo umeinyong’onyesha Simba, ambao walikuwa wakiigombania nafasi hiyo na Azam.
Kwa mantiki hiyo, Azam, mechi yao ya mwisho dhidi ya Mgambo itakuwa ni kuweka heshima tu na ilihali kwa Simba, haitakuwa na maana hata akishinda mechi yake ya mwisho.
Simba haitaweza tena kuifikia Azam, ambayo kwa ushindi wao dhidi ya Yanga, wamefikisha pointi 48, wakati Simba, hata akishinda mechi yake iliyobaki dhidi ya JKT Ruvu itafikisha pointi 47.
Ushindi huo, unaifanya Azam FC ifikishe pointi 48 baada ya kucheza mechi 25, nyuma ya mabingwa, Yanga SC wenye pointi 55 za mechi 25.
Azam FC ilitoka nyuma kwa 1-0 baada ya Mbrazil Andrey Coutinho kutangulia kuifungia Yanga SC dakika ya 12 na Bryson Raphael akasawazisha dakika ya 14 kabla ya Aggrey Morris kufunga la ushindi dakika ya 85.
Yanga, kwa kuwa mabingwa, wataiwakilisha Tanzania Bara katika Kombe la Washindi Afrika mwakani wakati Azam itashiriki kombe la Shirikisho na kuifanya Simba, moja ya klabu kongwe, kuwa nje ya mashindano ya kimataifa kwa zaidi ya miaka 3 mfululizo
Baada ya mechi hiyo, Yanga ilikabidhiwa kombe hilo mbele ya mashabiki, ambao hawakujali kipigo cha timu yao na kuwa kwa kuwa na furaha ya ubingwa

Post a Comment

 
Top