Wycliffe Kinyamal ameishindia Kenya medali ya dhahabu ya kwanza katika mbio za fainali za wanaume za mita 800, katika mashindano ya Jumuiya ya madola.
Aliyekuwa bingwa Nijel Amos wa Botswana, aliyemshinda David Rudisha miaka minne iliyopita, aliishia kuwa wa mwisho katika mchuano huo.
Mwenzake Kinyamal, kutoka Kenya, Jonathan Kitilit alishika nafasi ya sita, wakati Joseph Deng, wa Australia, aliyezaliwa kwenye kambi ya wakimbizi baada ya mama yake kukimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe Sudan, alishika nafasi ya saba.
Mwanariadha kutoka Afrika Kusini, Caster Semenya, anatarajiwa kupata medali ya pili ya dhahabu, baada ya kumaliza wa kwanza katika raundi ya kuingia katika fainali za mita 800.
Bara la Afrika linatarajia kupata medali zaidi baada ya wanamichezo watano:
- Eglay Nalyanya - Kenya
- Margaret Wambui - Kenya
- Emily Tuei - Kenya
- Docus Ajok - Uganda
- Winnie Nanyondo- Uganda
Post a Comment