0
Thomas TuchelHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionThomas Tuchel
Meneja wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund Thomas Tuchel anatarajiwa kuchukua nafasi ya meneja wa sasa wa Arsenal Arsene Wenger mwisho wa msimu. (Kicker - kwa Kijerumani)
Hilo lisipofanyika, Tuchel basi badala ya kwenda Arsenal atajiunga na Paris St-Germain ya Ufaransa, ingawa Chelsea bado wanazisaka huduma zake. (Sportbuzzer - kwa Kijerumani)
Wawakilishi wa Barcelona watakutana na wenzao wa Atletico Madrid siku chache zijazo kwa lengo la kukamilisha makubaliano kuhusu uhamisho wa nyota Mfaransa Antoine Griezmann, 27. (Sport - kwa Kihispania)
Kiungo wa kati wa Liverpool Mjerumani Emre Can, 24, ataihama klabu hiyo bila kulipiwa ada yoyote mwisho wa msimu huku Manchester City na Juventus wakidaiwa kumtaka iwapo klabu yake haitaongeza mshahara wake ambao kwa sasa ni £200,000 kila wiki. (Sun)
Antoine GriezmannHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Manchester United wanamtaka beki wa Scotland wa miaka 20 anayechezea klabu ya Celtic Kieran Tierney. (Daily Record)
Inter Milan nao wamewapiku Manchester City na Barcelona na kupata saini ya beki Mholanzi Stefan de Vrij, 26, ambaye atajiunga nao kutoka Lazio bila ada yoyote mwisho wa msimu. (Gazzetta dello Sport - Kwa Kitaliano)
Kiungo wa kati kinda wa Manchester City Phil Foden, 17, na kinda anayechezea Borussia Dortmund Jadon Sancho, 18, waliondolewa kwenye kikosi cha England cha wachezaji wa chini ya miaka 19 wanaocheza michuano ya ubingwa Ulaya baada yao kufika kwa mazoezi wakiwa wamechelewa. (Telegraph)
Scott SinclairHaki miliki ya pichaSNS
Image captionScott Sinclair
Brighton na Bournemouth wanamnyatia mshambuliaji Mwingereza anayechezea Celtic Scott Sinclair, 29. (Mail)
Swansea nao wanadaiwa kutaka sana kubadilisha uhamisho wa mkopo wa kiungo wa kati wa Wales Andy King, 29, kuwa uhamisho wa kudumu iwapo watanusurika na kusalia ligi kuu. (Mirror)
Kipa wa Manchester United na Uhispania David de Gea amesema mpira utakaotumiwa Kombe la Dunia baadaye mwaka huu "ni wa ajabu sana" na "ulihitaji maboresho". (AS)
David de GeaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Klabu za Ligi ya Premia zitachelewesha kuanza kutumia teknolojia ya video kuwasaidia waamuzi (VAR) kwa msimu mwingine mmoja kura itakapopigwa13 Aprili. (Mirror)
Mshambuliaji wa Tottenham Son Heung-min anaamini mwenzake klabu hiyo ya Spurs Harry Kane ndiye mchezaji bora zaidi duniani kwa sasa. (Sky Sports)
Mashabiki takriban 42,000 wanatarajiwa kuhudhuria kikao wazi cha mazoezi cha timu ya taifa ya Uhispania katika uwanja wa mazoezi wa Atletico Madrid wa Wanda Metropolitano Jumatatu. (AS)
Montpellier walitoa wito kwa FBI na French Ligue 1 kwa kutania wafike wachunguze ni kwa nini hawakupewa mkwaji wa penalti ligini katika kipindi cha mwaka mmoja. (Montpellier HSC kupitia Twitter)

Post a Comment

 
Top