Mshambuliaji Mfaransa anayechezea Atletico Madrid Antoine Griezmann anataka kujua hatima yake katika klabu hiyo kabla ya kusafiri kwenda kucheza Kombe la Ufaransa. Mchezaji huyo wa miaka 27 amehusishwa na kuhamia Barcelona. (L'Equipe kupitia Sky Sports)
Tottenham nao wanakusudia kutumia kifungu cha £3m kumfungua Jonny Evans kutoka kwa mkataba wake West Brom iwapo timu hiyo itashushwa daraja. Mchezaji huyo wa miaka 30 kutoka Ireland Kaskazini huenda pia akatafutwa na Arsenal. (Telegraph)
Juventus wamesitisha juhudi zao za kumtafuta beki kamili wa Uhispania anayechezea Arsenal Hector Bellerin, 23. Hii ni kwa sababu wana imani kwamba watafanikiwa kumchukua beki Mwitaliano Matteo Darmian, 28, kutoka kwa Manchester United. (Goal)
Mshambuliaji wa Arsenal Lucas Perez, 29, anataka kurejea katika klabu hiyo ya Ligi ya Premia baada ya kutofanya vyema akiwa kwa mkopo Deportivo La Coruna. Mhispania huyo alizomewa na mashabiki majuzi baada yake kuendelea kutofanya vyema. (Independent)
Kipa wa Atletico Madrid na Slovenia Jan Oblak amesema hana uhakika iwapo atasalia katika klabu hiyo msimu ujao. Arsenal wanataka sana mlindalango huyo wa miaka 25 ajiunge nao kuchukua nafasi ya Petr Cech, 35, atakapostaafu. (London Evening Standard)
Kipa wa Chelsea kutoka Argentina Willy Caballero, 36, atasalia katika klabu hiyo hadi Juni 2019. Hata hivyo, kipa wao nambari wani Thibaut Courtois, 25, bado anaweza kuihama klabu hiyo. Courtois mkataba wake utafikia kikomo mwisho wa msimu. (Goal)
Kiungo wa kati wa zamani wa Italia Andrea Pirlo huenda akapewa kazi yake ya kwanza kabisa ya ukufunzi katika timu ya taifa iwapo mmoja kati ya Carlo Ancelotti na Antonio Conte ndiye atapewa kazi ya kuwa meneja wa timu ya taifa. (Gazzetta dello Sport kupitia Football Italia)
Paris St-Germain wanataka kocha wa Juventus Massimiliano Allegri ajiunge nao kumrithi Unai Emery mwisho wa msimu. (ESPN)
Bingwa wa Olimpiki mara nane Usain Bolt atafanya mazoezi na klabu ya Borussia Dortmund inayocheza Bundesliga katika kikao cha mazoezi ambacho kitakuwa wazi kwa umma. (Yahoo Sports)
Kiungo wa kati wa Bournemouth Lewis Cook, 21, atajishindia £17,000 kutoka kwa babu yake iwapo atateuliwa kuchezea England dhidi ya Uholanzi au Italia. (Yorkshire Evening Post)
Na beki wa Stoke mwenye miaka 29 Erik Pieters kutoka Uholanzi ameomba radhi baada yake kuvunja amri ya kutotoka nje kwenda kwa burudani katika kilabu kimoja kabla ya mechi ya Stoke na Everton wikendi iliyopita. (Stoke Sentinel)
Post a Comment