0

 Mchezaji wa timu ya Kigamboni fc akijaribu kuuzipiti mpira mbele yake kwenye mchezo dhidi ya timu ya Mitumba fc katika mchezo huo Kigamboni fc walikubali kichapo cha magoli 3-1 mchezo uliochezwa uwanja wa wilaya ya Liwale.
Lango la timu ya Kigamboni fc likishambuliwa 




Ligi la Alizeti cup 2017 leo septemba 12 kulikuwa na  mchezo kati ya Mitumba fc dhidi ya Kigamboni fc umemalizika baada ya Mitumba fc kuibuka na ushindi mnono wa magoli 3-1 mchezo ulipigwa katika uwanja wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Katika dakika 45 za kipindi cha kwanza timu ya Mitumba fc iliweza kuongoza magoli 2-0,magoli hayo yalipatikana dakika za mwanzoni mwa mchezo baada ya safu za mabeki wa Kigamboni kushindwa kulinda kuta zao na kuweza kurusu magoli mawili.

Kipindi cha pili timu ya Kigamboni fc iliweza kusoma mchezo waliokuwa wanacheza Mitumba fc na waliweza kupata goli lililofungwa na Tamimu Komogo namo dakika ya 70 kwa mkwaju wa penaiti  na Mitumba fc katika kipindi cha pili waliongeza goli.

Magoli ya Mitumba fc yakifungwa na Salumini Mwaska dakika ya 10,Haikosi Mpwate dakika ya 20 na goli la Ramadhani Milyango ikifungwa kwa mkwaju wa penaiti baada ya mlinda mlango wa Kigamboni kumchezea faulo mchezaji wa Mitumba fc ndani ya boksi.

Kwa upande wake kocha Kigamboni fc,Imamu Mahuru akizungumza na mwandishi wetu alisema walicheza vizuri japo wameweza kupoteza mchezo huo lakini hawajakata tamaa nae kapteni wa Mitumba fc,Shabani Mbwani  alisema mchezo ulikuwa mzuri licha ya kuwa na changamoto japo hawajajiandaa vizuri .

Kesho septemba 13 katika kituo cha Liwale mjini kutakuwa na mchezo kati ya Vijuso fc dhidi ya timu ya Changamka fc mchezo utakao chezwa katika uwanja wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale.

Mashindano haya ya Alizeti cup 2017 yanazaminiwa na chama cha ushiriki cha Umoja Amcos yakiwa na lengo la kuibua vipaji pamoja na kuwahamasisha wakulima wilayani hapa kulima zao la alizeti ili kuongeza kipato na kauli mbiu “Liwale alizeti ni fedha” 

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top