Image captionWabunge wametakiwa kukutana katika kikao cha dharura ili kujadili hatma ya rais Mugabe
Chama tawala cha Zanu-Pf nchini Zimbabwe kimewataka wabunge wake kukutana na kujadili hatma ya rais Robert Mugabe, baada ya siku ya mwisho ya yeye kujiuzulu kupita.
Siku hiyo iliwekwa na chama cha Mugabe cha Zanu-Pf .
Mugabe anatarajiwa kujadiliwa bungeni kuanzia siku ya Jumanne ambapo anakabiliwa na shtaka la kumuachia mkewe kuwa na mamlaka ya kikatiba kulingana na chama tawala cha Zanu-Pf.
Kiongozi huyo anayepigwa vita aliwashangaza raia wengi wa Zimbabwe siku ya Jumapili alipotangaza katika runinga kwamba angependa kusalia kuwa rais.
Zanu-Pf kimesema kuwa kinaunga mkono hatua ya kuhoji uhalali wa rais Mugabe kuwa rais wa taifa hilo na kwamba mipango ya kumchukulia hatua hiyo inaweza kuanza siku ya Jumanne wakati bunge litakapokutana.
Katika muswada ulioonekana na kituo cha habari cha Reuters's chama hicho kimemlaumu rais huyo kwa kuharibu uchumi wa taifa hilo.
Uwezo wa rais Mugabe umepungua tangu jeshi kuingilia kati Jumatano iliopita kuhusu mzozo wa ni nani atakayemrithi.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionBunge latakiwa kujadili hatma ya Mugabe Zimbabwe
Mgogoro huo ulianza wiki mbili zilizopita wakati kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 alipomfuta kazi makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa na hivyobasi kuwakasirisha makamanda wa jeshi ambao waliiona hatua hiyo kama ya kujaribu kumfanya mkewe kuwa mrithi wake.
Taifa hilo limeshuhudia maandamano makubwa ya kumtaka rais Mugabe kujiuzulu mara moja.
Kupitia safu yetu ya mahusiano, leo nimekuletea makala maalum hasa kwa wanawake kutokana na malalamiko ya wanawake wengi kuwapoteza waume zao. Ki...Read more »
kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja kumfahamu mwenzake, lakini kuzoeana huku kunaweza kuzalisha dharau hususani kwa...Read more »
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionHuenda ndege zikatengezwa bila madirisha katika siku za usoni.
Kampuni ya ndege ya Emirates imezindua nd...Read more »
Image captionMaandamano yamefanyika mjini Nairobi siku ya Jumatatu kulalamika kuhusu tuhuma za ubakaji katika shule ya Moi Girls Nairobi
Walimu pamoj...Read more »
Operesheni ya mwisho ya Tundu Lissu imefanyika na kumalizika salama.
Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alifanyiwa op...Read more »
Haki miliki ya pichaAFPImage captionBado muswada unahitaji kupitishwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kufanya kazi.
Bunge nchini Rwanda...Read more »
Post a Comment
aprieztmkrdezign
218168578325095
Emoticon
Click to see the code! To insert emoticon you must added at least one space before the code.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.