0
Wezi wachimba handaki na kuiba milioni 50 za benki Kenya
Image captionWezi wachimba handaki na kuiba milioni 50 za benki Kenya
Maafisa wa polisi wanachunguza wizi wa shilingi milioni 50 uliofanyika katika tawi moja la benki ya KCB mjini Thika nchini Kenya.
Kufuatia kisa hicho kamanda wa polisi katika kaunti ya Kiambu Adiel Nyange amesema kuwa watu watatu wamekamatwa.
Kulingana na polisi hao, majambazi hao waliingia katika chumba cha kuhifadhi fedha cha benki hiyo kupitia handaki walilochimba chini ya ardhi na kuiba fedha hizo ambazo zilikuwa zimehifadhiwa ndani ya chumba hicho.
Wanaaminika kukata masanduku mawili ya kuhifadhia fedha hizo kwa kutumia mwako wa moto.
Polisi wanasema kuwa meneja wa benki hiyo aligundua kwamba benki hiyo imeibiwa muda wa saa mbili alfajiri wakati alipofungua chumba hicho cha kuhifadhia fedha.
''Majambazi hao lazima walikuwa na mtu anayefanya kazi katika benki hiyo aliyewaongoza hadi pale masunduku hayo yalipokuwa. Uchunguzi unaendelea'' , alisema naibu wa kamanda wa polisi Bernard Ayoo.

Post a Comment

 
Top