0

Bunge limeazimia waziri wa nishati na madini Mhe.Prof Sospeter Mhongo,Waziri wa ardhi Prof. Anna Tibaijuka,Mwanasheria mkuu wa serikali jaji Fredrick Werema na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini pamoja na bodi ya wakurugenzi wa Tanesco wawajibishwe kwa kuishauri mamlaka ya uteuzi  kutengua uteuzi wao.
Akiwasilisha maazimio hayo mwenyekiti wa PAC Mhe. Zitto Kabwe amesema bunge pia linapendekeza serikali kuangalia uwezekano wa kuinunua mitambo ya IPTL na kuikabidhi kwa Tanesco,pamoja kamati za kudumu za bunge zichukue hatua za haraka kabla ya mkutano wa 18 wa kuwavua nyazifa zao wenyeviti wa kamati za bunge waliotajwa kuhusika na kashfa mabilioni ya fedha katika za Escrow.
 
Kwa upande wake kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ni Mhe. Freeman Mbowe  amewata viongozi kutambua kuwa wanamamlaka ya kulinda rasilimali za nchi na kumtaka waziri mkuu kuwa mkali zaidi kwa kuchukua hatua na asisubiri mpaka bunge lifikie katika hatua ya mivutano,huku makamu mwenyekiti wa kamati ya PAC Mhe. Deo filikunjombe amepongeza  bunge kukubali kamati hiyo. 
 
Waziri wa nchi ofisi ya Rais mahusiano na utaribu Mhe.Stephen Wassira amesema jambo lolote linaloweza kuvunja umoja na kurudisha nyuma maendeleo haliwezi kuwa sera  ya CCM ambapo amepongeza makubaliano yaliyofikiwa  kati ya CCM na vyama vya upinzani.
 
Akihitisha mkutano wa 16 na 17, waziri mkuu mheshimiwa mizengo pinda amewahakikishia wabunge na wananchi kwa ujumla kuwa serikali itaendelea kusimamia rasilimali za nchi kwa faida ya watanzania wote, na kuahidi wale wote watakao patikana na jinai za kuvunja sheria za nchi watachukuliwa hatua.Ambapo ameahirisha bunge hadi tarehe 27 januari mwakani.ITV

Post a Comment

 
Top