0
                       Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amemtaka Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamadi (pichani), ajiuzulu nafasi hiyo kwani iko chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho amekuwa akikitukana kwa madai kuwa hakifai.
 
Amesema ni vyema akabaki na kazi ya kupinga kwa ajili ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) badala ya kukitukana chama ambacho ndicho kilichomuweka madarakani. 
 
Nape alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara, mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhaman Kinana, katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua, kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010/2015. 
 
"Maalim Seif aachie ngazi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ili afanye kazi ya Ukawa ambayo haina lolote.Wameanza kutofautiana kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa,"alisema.
 
Alisema, Maalim Seif ambaye anazunguka na kuwaambia wananchi kuwa CCM mbaya ni kuwahadaa Watanzania kwani kwa sasa maisha yake yanaendeshwa na serikali ya chama hicho ambacho ndicho kinamlipa mshahara.
 
Alisema, CCM haiko tayari kuacha wapinzani wakaenda Ikulu kwani Ikulu kinakwenda chama cha siasa na siyo makundi ya wanaharakati. 
"CCM inaweza kucheza na wapinzani katika maeneo mbalimbali lakini si kwa kuwaacha washinde nafasi ya urais, ubunge na udiwani. Kifupi upinzani hauwezi kwenda Ikulu," alisema Nape.
 
Alifafanua kuna tofauti kubwa kati ya CCM na wapinzani kwani CCM, wanazungumzia maendeleo ya wananchi na wapinzani wanazungumza porojo na kejeli na kutengeza chuki dhidi ya Watanzania.
                                         CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

 
Top