0


Matokeo ya mchezo wa hatua ya nusu fainali katika kituo cha Liwale mjini,timu ya Hawili FC ambao mabingwa  watetezi wa Ligi ya Alizeti cup jana octoba 2 waliitembezea kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Kigamboni FC na kujihakikishia kutangulia hatua ya fainali kwenye Uwanja wa Halmashauri ya wilaya Liwale mkoani Lindi. 


Katika kipindi cha kwanza timu ya Hawili fc iliweza kuongoza magoli 2-0 na katika kipindi cha pili Hawili fc iliweza kuongeza goli baada ya Kigamboni fc kupata goli moja.

magoli ya Hawili fc yalifungwa na Ramadhani Hashimu dakika ya 3,Huseni Mchite dakika ya 40 na goli la tatu likifungwa na Imani Mbeswige katika dakika ya 80 na goli la Kigamboni likifungwa na Dickson Fidels namo dakika ya 70

Timu ya kigamboni itangoja mchezo wa kumpata mshindi wa nafasi ya tatu itacheza na timu itakayofungwa leo octoba 3.

Leo octoba 3 kutakuwa na mchezo wa nusu fainali kati ya aliongoza kundi B na mshindi wa pili wa kundi B ambapo kutakuwa na mchezo kati ya Mitumba fc Vs The youth Fighter fc mchezo unaotarajia kuwa mkali.

KUWA MTU WA KWANZA KUPATA HABARI LIKE PAGE KWA KUBOFYA>> hapa

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top