0

Rais Dkt John Magufuli amesema hawezi kuwasaliti watanzania katika kipindi chake chote cha kuongoza nchi alichopewa na watanzania

Rais Magufuli amesema hakuna vita ngumu kama ya uchumi ambayo anaendelea nayo sasa hasa ya kupigania rasilimali za nchi ikiwemo madini yanayoporwa na kuachia taifa umasikini

Amesema kwa kuwa maechaguliwa kuwa Rais katika kipindi chake chote cha uongozi wake hakuna wa kuichezea Tanzania

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika mkutano wa ALAT jijini Dar Es Salaam


Rais Magufuli: Na mimi nataka niwahakikishie katika awamu hii chini ya uongozi wangu, hakuna kuchezewa. 

Rais Magufuli: Hakuna nchi ambayo mnaona rasilimali zinachukuliwa alafu mkanyamaza tu mkachekelea, tumechukua hatua. 

 "Kwa siku chache baada ya kudhibiti uzalishaji wa Tanzanite umeongezeka zaidi ya mara 30"-Rais @MagufuliJP


Rais Magufuli: Ndio maana kwenye Tanzanite tumeamua kujenga uzio
- Na gharama ya uzio haizidi hata Bilioni 6

 "Fedha zote zilizokusanywa kutokana na Tanzanite duniani, Tanzania imepata asilimia 5 tu"-Rais @MagufuliJP

Post a Comment

 
Top