Mtanange mkali wa Kufungua Pazia Msimu Mpya wa Soka wa 2017/18 hapa Tanzania Bara kwa kugombea Ngao ya Jamii kati ya Mabingwa wa VPL, Yanga na Simba mabingwa wa FA CUP, umemlizika augosti 23 mwaka 2017 kwa Simba kuwa kidedea kwa Mikwaju ya Penati 5-4 zilizopigwa baada ya Sare ya 0-0 ya Dakika 90 za Mchezo.
Mchezo huo ambao ulianza majira ya saa kumi na moja kamili za jioni katika Dimba la Uwanja wa Taifa, kivutio kikubwa katika mchezo huo walikuwa wachezaji wapya ambao wamesajiriwa na timu hizo kwa msimu huu wa mwaka 2017/18 hasa hasa ni Haruna Niyonzima wa Simba na Papy Kabamba Tshimbi wa Yanga ambao wameweza kuonyesha kandanda safi.
Kipa Mcameroon wa Yanga, Youthe Rostand aliokoa penalti ya beki wa kushoto na Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, lakini akashindwa kuokoa za beki Mzimbabwe, Method Mwanjali, mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi, kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, na wazawa Shiza Kichuya na Mohammed Ibrahim ‘Mo’.
Kwa Simba hiyo inakuwa mara ya tatu kutwaa Ngao ya Jamii tangu ilipoanzishwa mwaka 2001, baada ya kuibeba pia katika miaka ya 2011 ikiifunga Yanga pia 2-0 na 2012 ikiifunga Azam FC 3-2.
VIKOSI VILIVYOANZA: YANGA: Youth Rostand, Juma Abdul, Gadiel Michael, Andrew Vincent, Kelvin Yondani, Pappy Tshishimbi, Raphael Daud, Thaban Kamusoko, Donald Ngoma, Ibrahim Ajib, Emmanuel Martin
Akiba: Ramadhan Kabwili, Hassan Kessy, Haji Abdallah, Mwinyi Haji, Juma Makapu, Yusuph Mhilu, Juma MahadhiSIMBA: Aishi Manula, Ally Shomari, Erasto Nyoni, Salim Mbonde, Method Mwanjali, James Kotei, Shiza Kichuya, Muzamiru Yassin, Laudit Mavugo, Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima
Akiba: Emmanuel Mseja, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Juma Liuzio, Juuko Murushid, Mahamed Hussein, Mohamed Ibrahim
REFA: Hery Sasii [Dar es Salaam]
Post a Comment