#AJALI
Watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya daladala waliokiwa wakisafiria kugonga #treni na kubuzwa umbali wa mita zaidi ya 15 mkoani Morogoro.
Watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya daladala waliokiwa wakisafiria kugonga #treni na kubuzwa umbali wa mita zaidi ya 15 mkoani Morogoro.
Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Ulrich Onesphory Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema taarifa zaidi itapatikana baadae.
Taarifa kamili juu ya ajali
Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linamshikilia dereva wa basi lenye namba za usajili T 438 ADR Charles Diamond, kwa kusababisha ajali iliyopoteza uhai wa watu mkoani Morogoro na kusababisha majeraha kwa baadhi ya watu.
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Ulrich Matei
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Ulrich Matei
Akitoa taarifa ya ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi Kamanda wa Polisi mkoani humo Urlich Matei, amesema mpaka sasa idadi kamili ya watu waliofariki kutokana na ajali hiyo ni watu watatu, ambapo wawili ni wanawake na mmoja ni mwanaume, huku mmoja wao akiwa ni mwanafunzi.
Majeruhi wa ajali hiyo ni 27 ambao wamepelekwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, lakini suala la utambuzi wa miili ya marehemu bado halijafanyika mpaka pale uchunguzi utakapofanyika.
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi iliyohusisha gari aina ya daladala ikielekea Mvumi kugonga treni iliyokuwa ikipita kwenye njia yake, kulikopelekea kuburuzwa kwa gari hiyo na kusababisha vifo
Post a Comment