GERMANY, Mabingwa wa Dunia, wameanza vyema Mechi yao ya Kundi B la Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara iliyochezwa huko Fisht Stadium, Mjini Sochi, Nchini Russia, kwa kuibwaga Australia 3-2.Hadi Mapumziko Germany waliongoza 2-1 kwa Bao za Lars Stindl, Dakika ya 5, na Julian Draxler, Penati ya Dakika 45, wakati Australia wakifunga Bao lao Dakika ya 41 ambalo alifunga Tom Rogic.
Kipindi cha Pili, Germany walipiga Bao la 3 Dakika ya 48 Mfungaji akiwa Leon Goretzka lakini Australia wakapata Bao la Pili Dakika ya 58 kupitia Tomi Juric.
Kesho Jumanne ni Mapumziko na Jumatano zipo Mechi 2 za Kundi A ambapo Wenyeji Russia wataanza na Portugal na kufuatia Mexico na New Zealand.
VIKOSI: Australia: Ryan; Degenek, Sainsbury, Wright; Leckie, Milligan, Mooy, Behich; Luongo, Rogic; Juric
Germany: Leno; Kimmich, Mustafi, Rudiger, Hector; Goretzka, Rudy, Stindl; Draxler, Brandt, S. Wagner
REFA: Mark Geiger (USA)
Post a Comment