0


MWENYEKITI wa kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma, amelishauri shirika la Bandari Zanzibar, kuandaa utaratibu wa kutafuta eneo kwa ajili ya kujenga chelezo ya kuzifanyia matengenezo, vyombo mbali mbali vya baharini  pindi vinapopata hitilafu.

Ametoa ushauri huo mara baada ya kupata taarifa ya bandari ya Wesha, kutoka kwa Mkurugenzi wa bandari kisiwani Pemba, wakati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea bandari hiyo iliyopo Chake Chake Kusini Pemba.
Mhe. Hamza ambaye ni mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura, amesema ni jambo la kusikitisha kuiona Serikali, inashindwa kujenga chelezo yake kisiwani Pemba, jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya bandari.
Nae Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, ambaye ni mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake Mhe. Suleiman Said Sarahani, amesema shirika la Bandari Pemba, linapaswa kuhakikisha wanalipima eneo lao na kuweza kuwa na
hatimiliki, kwa lengo la kuondosha uvamizi katika maeneo ya
taasisi za Serikali.
Bandari ya Wesha imekuwa ikipokea mizogo tani 200 hadi 400 kwa mwezi, kutoka vyombo vidogo vidogo vinavyotoka Tanga na kukusanya mapato kati ya shilingi Milioni 4 hadi milioni 5 kwa mwezi.


Post a Comment

 
Top