Watendaji wa taasisi mbali mbali
za Serikali na binafsi visiwani Zanzibar wametakiwa kuwaenzi na kuwathimini wazee wanaoishi
kwenye nyumba za kulelea wazee Zanzibar.
Hao
ni miongoni mwa Wazee wanaoishi katika
nyumba ya kulelea wazee Welezo Zanzibar
Mwenyekiti wa kamati ya mifugo, utalii,
uwezeshaji na habari ya baraza la wawakilishi Mhe. Ali Suleiman Shihata ambae
pia ni mwakilishi wa jimbo la Kijitoupele ameyasema hayo kwenye ziara ya kamati
hiyo katika nyumba ya wazee Sebuleni.
Amesema kuwasaidia wazee ni jambo muhimu
kutokana na mchango walioutowa katika taifa.
Mhe.
Shihata ameagiza kuwepo usafiri kwa saa 24 kwenye kituo cha Sebuleni ili
kuwasaidia wazee inapotokea dharura.
Pamoja
na hayo ametaka kuorodheshwa familia za watu
wanaoishi katika mazingira magumu ili kuwapatia huduma muhimu ikiwemo
makazi, malazi na chakula.
Nae mkurugenzi
wa wizara ya kazi, uwezeshaji,vijana, wazee, wanawake
na watoto, amesema wizara
yake ina majukumu mengi
lakini asilimia kubwa ya
majukum hayo wameshayatekeleza ikiwemo kusaidia familia 95 wanaoishi katika mazingira magumu.
Na kuwapatia posho wazee wenye miaka 70
na kuendelea, mfumo ulianzishwa tareh 15/4/2016 ambapo mpaka kufikia Disemba 2016 wazee waliosajiliwa
ni 16 elfu, mia 8 na 35 kisiwani Unguja.
Post a Comment