Wazazi visiwani Zanzibar wametakiwa kuwa karibu na watoto hasa wenye
ulemavu kwa lengo la kuwakinga dhidi ya vitendo vya unyanyasaji na ukatili unaofanywa na baadhi ya watu hapa nchini.
Katibu mkuu kutoka
jumuiya ya wasiona Zanzibar Adil Muhammed Ali ametoa rai hiyo alipokuwa
akizungumza na mwandishi wetu , amesema watoto wenye ulemavu wanahitaji ulinzi mkubwa
ili nao waewze kufikia malengo yao.
Ameongeza kuwa licha ya
serikali kupiga vita vitendo vya udhalilishaji lakini bado vimekuwa vikiendelea
kushamiri na kuzusha hofu ndani ya jamii.
Pamoja na hayo Adil
ametoa wito kwa majaji kuwa makini wakati wa kutowa hukumu dhidi ya kesi
zinazowahusu watoto wenye ulemavu kutoa
na baadhi yao kushindwa kutoa ushahidi kwa ufasaha kutokana na ulemavu
walionao.
Post a Comment