Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anatarajiwa kuzozana na maafisa wakuu wa klabu hiyo kuhusu bajeti yake ya uhamisho huku joto la wasiwasi likipanda katika klabu hiyo, Paris St-Germain huenda ikamshawishi kuhamia Ufaransa. (Mirror)
Mourinho ameamua kuhusu kuwanunua wachezaji wanne huku wachezaji saba katika kikosi chake cha sasa wakitarajiwa kuuzwa.
United imetaka kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Willian mwisho wa msimu huu huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akitarajiwa kugharimu £60m. (Sun)
- Conte asema Chelsea kuchapwa 3-0 na Barcelona haikuwa haki
- Chelsea yatupwa nje na Barca michuano ya UEFA
- Mourinho: Man Utd kuondolewa UEFA si jambo geni
Mkufunzi wa Leicester Claude Puel anatarajiwa kupewa dau kubwa la ununuzi wa wachezaji mwisho wa msimu huu .(Leicester Mercury)
Chelsea ina hamu ya kumsajili beki wa Juventus na Ghana Kwadwo Asamoah ,29, kwa uhamisho wa bure wakati kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu huu (Sun)
Bayern Munich na Juventus zina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool na Ujerumani 24- Emre Can (Mirror)
Vitesse Arnhem inataka kumpatia kandarasi ya kudumu kiungo wa kati wa Uingereza Mason Mount ,19, kwa msimu mwengine. (VL - in Dutch)
Manchester City inatarajiwa kutia saini kandarasi yenye thamani ya £45m kwa mwaka na kampuni ya Puma. Kandarasi yao na kampuni ya Nike ina thamani ya £18m kwa mwaka. (Sun)
Mshambuliaji wa Liverpool mwenye umri wa miaka 17 Rhian Brewster ataanza kushirikishwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo wakati atakapopona jeraha alilopata msimu ujao.. (Telegraph)
Beki wa Burnley James Tarkowski 25 anatarajiwa kupokea wito wake wa kwanza katika timu ya Uingereza. (Times - subscription required)
Fifa imepanua uchunguzi wake kuhusu iwapo Manchester City ilivunja sheria kuhusu usajili wa wachezaji.
Klabu hiyo huenda ikaadhibiwa na marufuku ya uhamisho iwapo itapatikana na makosa. (Telegraph)
Afisa mkuu wa klabu ya Atletico Madrid Miguel Angel Gil alilazimika kulala ndani ya hoteli ya uwanja wa ndege wa mjini Moscow kwa kuwa hakuweza kupata pasipoti yake alipowasili kutoka Uhispania siku ya Jumanne.. (El Pais - in Spanish)
Mchezaji wa Stoke aliyevunja rekodi ya usajili katika klabu hiyo Giannelli Imbula ameshirikishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo , ikiwa ni mara yake ya kwanza kushirikishwa na timu hiyo..
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 yupo kwa mkopo katika klabu ya Ufraansa ya Toulouse. (Stoke Sentinel)
Mshambuliaji wa Tottenham Son Heung-min huenda akakosa mwazo wa msimu ujao iwapo Korea Kusini itaamua kumshirikisha kama mmojawapo ya wachezaji watatu wenye umri wa wastani katika kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 kwa michezo ya bara Asia.. (Evening Standard)
Mkufunzi wa West Ham David Moyes aliwatetea wachezaji wake wakati wa likizo yao mjini Florida wiki hii licha ya pingamizi kutoka kwa bodi ya timu hiyo. (Mirror)
Post a Comment