SEHEMU YA SITA
“Kajina maisha yako yapo hatarini kwa kiasi
kikubwa, kuwa mbali kabisa na viumbe vinavyoitwa wanawake,.. kaa mbali kabisa”
kwa ukali sana sauti ile ilipitia nikiwa bado angali niko usingizini.
Nilishituka kutoka usingizini kwa hali
ya kugofya sana huku moyo wangu ukienda mbio vibaya.
Nilijishangaa kwa nini hali ile
inanijia na inahusiano gani na maisha yangu? au kuna jambo zito ambalo
linakwenda kunitokea katika maisha yangu. Nilijiuliza huku nikijipatia majibu
ya maswali yangu. Nilijionya mwenyewe huku nikijisema, “haiwezekani hata kidogo!”.
Machungu ndani ya moyo wangu
yaliongezeka maradufu sikujua mwisho wa yote utakuwa nini?, kama chanzo bado
kinanitatiza je huko mwisho kutatokea nini?. Bado hali ile iliniacha kwenye
taharuki kali ndugu msikilizaji wasimulizi hii. Hakika kama kunajambo baya
ambalo ningelijua mapema, lilikuwa linaenda kunitokea ndani ya maisha yangu,
basi ningeliziua kuanzia pale.
********
"Criss… Criss!, mwanangu upo
kweli wewe au umelala asubuhi yote hii,” nikiwa bado nipo kimya sauti ya mama ilizidi
kupenya kwenye vitundu vya masikio yangu, ikinitaka kuamka katika asubuhi ile,
ikiwa mwanga wa jua, ulishaanza kuipendezesha siku katika namna nyingine.
Niliitika ilikumjulisha kuwa nimeamka,
wakati nikijivuta kivivu kutoka kitandani, ndipo niliposikia sauti ya mama tena
ikinitaka nitoke nje.
Nilinyanyua nikitokea pale huku macho
yangu yakiwa bado hayajatoka na wenge la usingizi. Miale ya jua nayo
ilinikabili punde na kuninyanyasa pindi nilipotoka nje, nilihisi macho yangu
kuwa mazito vibaya hata sikuelewa nini kimenikumba, ila nilianza kusikia
maumivu kidogo kidogo kutoka kwenye mboni zangu. Nikiwa tayari nimemfikia mama
yangu pale alipokuwa amekaa.
Maneno ya mama tu yalitosha kusawili
kile nilichokuwemo kwenye macho yangu. “Kulikoni mwenzetu mbona macho yamevimba
ulikuwa unalia nini usiku kucha?” . Mama alinuliza huku akiendelea kunitandika
swali lingine wakati hata sijajibu, “au una tatizo ila unaonekana haupo sawa baba
yangu hata kidogo?”.
Maneno yale niliyasikia vizuri, wakati
huo nipo kimya hata cha kujibu sina. Maneno yake yalinitia uchungu sana grafla
nikakumbuka tukio lilotokea muda mfupi kabla sijapitiwa na usingizi usiku wa
kuamkia siku hiyo.
Nilijikuta machozi yakianza
kunitiririka na kufatiwa na neno ambalo niliweza kulitamka kwa wakati huo. “Kwanini mama?,’’ linanitoka kwa gadhabu ya
hali ya juu. Hali yangu ilionekana wazi
kwenye mboni za mama kuwa haikuwa ya kawaida hata kidogo.
Hapo sasa hata maneno ambayo
niliyokuwa nikayatamka yalishindwa kutoka vizuri kwenye kinywa changu. Kwikwi zilifatia
ikiendana na kilio cha uchungu nilichokuwa na kitoa.
Hakika nilitamani dunia mzima kusiwe na wanawake ndani ya asabuhi ile, huku nikimpa nafasi ya upendeleo mama yangu. Nikiamini yeye pekee yake ndio alikuwa akistahiri kuwepo katika dunia kuliko viumbe hivyo.
Na hata kwenda mbali zaidi huku
nikiombea kama ikitokea vita hivi karibuni katika dunia basi viumbe hivyo
viteketezwe kabisa maana vina roho mbaya, ilo jaa chuki, usaliti tu kwenye mioyo
yao. Wanapenda kujijali wao tu na si
wenzao hata kidogo, watu wanamna hii hawafai hata kidogo.
Nijisemea ndani ya fikra zangu kimya kimya huku nikiambatanisha na kilio kizito
________
Baada ya muda mrefu kidogo hasira
zangu zilipungua na kasi ya kilio nacho nilichokuwa na kitoa kilipungua na
hatimaye mama alifanikiwa kuninyamazisha. Na kutoa kauli iliyopenya vyema
kwenye milindimo ya ngoma za masikio yangu, “aah hakika mama wee!,” nilimpa
haki yake kwenye kinywa changu kimoyo moyo kabla ya kuendelea kuongea.
"Mwanangu nakupenda sana wewe ndio baba yangu si pendi nikuone unasononeka juu ya jambo lolote lile. Haya kwanza naomba uniambie nini kinakutatiza wewe maana nakuona haupo sawa kabisa?”, aliniuliza mama huku akiendelea tena kuongea. “Na kama kuna jambo linakusumbua wazi wazi ndani ya kichwa chako na omba uniweke wazi!” aliongea kwa msistizo.
"Mwanangu nakupenda sana wewe ndio baba yangu si pendi nikuone unasononeka juu ya jambo lolote lile. Haya kwanza naomba uniambie nini kinakutatiza wewe maana nakuona haupo sawa kabisa?”, aliniuliza mama huku akiendelea tena kuongea. “Na kama kuna jambo linakusumbua wazi wazi ndani ya kichwa chako na omba uniweke wazi!” aliongea kwa msistizo.
Nilimsikiliza kwa makini yale maneno
ya mama, huku nikiteta na moyo wangu nikiamini wazi kuwa mama yangu ni mtu
mwenye upendo na mimi sana.
Wakati huo nilitulia kimya,
nikijishauri niweze kumwambia kilichokuwa kinanitatiza, niliona siku zote
mficha maradhi mauti siku moja umuumbua. Nilijikaza kisabuni kunyanyua mdomo wangu
ulionekana una mengi ya kuongea mbele ya macho ya mama na masikio yake, huku mama
akivuta umakini kupokea maneno yangu haswa.
"Mama maisha yangu yamekuwa
hayapo sawa kabisa siku hizi mbili tatu, namkumbuka sana kaka Eddy mpaka leo,
bado kaka Eddy ajanitoka hata kidogo nashindwa kumsahau kabisa yote kutokana na
maisha tuliyokuwa tunaishi. Upendo wake kwangu ulikuwa zaidi ya vyote mama”, nilisita
kidogo nikitazama kwa makini mama jinsi alivyokuwa akiyapokea yale maneno
yangu, kabla ya kuendelea kuzungumza. “Angalia mama, hata vitabu vya dini
vinasema tunatakiwa kusahau jambo ambalo limepita lakini kwangu imekuwa tofauti
kabisa,
angalia miaka kumi na kitu sasa.
Lakini nimekuwa mgumu sana kusahau jambo linanitesa sana sijui kwa sababu
tulizaliwa wawili?”, Nilimuliza mama swali la kizembe wakati nikiendelea kuongea,
niliona hilo alikuitaji majibu niliendelea kuzungumza huku nikijijibu mwenyewe.
Hilo sio tatizo mama upendo wake ndio
tatizo sidhani kama atatokea kaka kama yule kwenye maisha yangu.
Hakika kaka Eddy alikuwa mtu bora sana
kwenye maisha yangu si kwangu tu mama, hata wewe kwako!.
Mama aliendelea kunisikiliza kwa makini mno na namna yale maneno yalivyokuwa yakinitoka ndani ya kinywa changu, yalionekana yalikuwa yakimchoma mama na kumkumbusha mbali.
Niliendelea kuongea ila hali ya mama
alianza kuwatofauti kidogo kidogo, katika namna ambayo sikuitegemea kabisa
ndugu msikilizaji.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.