Je, unakumbuka picha za mwalimu huyu,Owura Kwadwo.
Mwezi uliopita mwalimu huyu alivuma mtandaoni baada ya kuweka picha akichora programu ya Microsoft Word kwenye ubao wakati wa darasa la tarakilishi.
Iligundulika kwamba alifanya hivyo kwa sababu shule anayofundishia haikuwa na tarakilishi za kuwafundushia wanafunzi somo hilo la kompyuta.
Alisema "kufundisha somo la kompyuta nchini Ghana inachekesha.
Sasa mwalimu huyo anahudhuria mkutano wa walelimishaji wa Microsoft unaofanyikia nchini Singapore.
Ameandika katika ukurasa wake wa Facebook, "Nimefika nchini Singapore katika mkutani wa Microsoft Global Education Exchange, Ninatarajia kujifunza mengi. Asante Microsoft.
Baada ya picha yake Owura Kwadwo kusambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter, kampuni ya Microsoft ilivutiwa na mwalimu huyo na kumpatia msaada wa vifaa vya kumsaidia katika kazi yake.
Post a Comment