0
Siri yafichuka Afande Sele Kujiunga na CCM


Msanii mkongwe wa BongoFleva nchini Afande sele atangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) mwezi huu march  mbele ya Rais Dkt. Magufuli kwa lengo la kuunga mkono jitihada zake anazozifanya katika kupigania na kukiomba chama kimpokee kama kijana wao.


Afande Sele ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anatumbuiza muziki kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro walioweza kuhudhuria shughuli za uzinduzi wa kiwanda cha Sigara mkoani humo na Rais Magufuli.

"Nataka nimuhakikishie Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kwamba mimi ni mtu wakufikiri, mbishi na mgumu sana katika kukubali jambo fulani lakini niseme kwa uwazi kabisa tangu ulipochukua madaraka ya kuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM umeweza kuinyosha nchi na kukisafisha chama chako na kimeweza kurudi katika uhimara wake kama alivyokuwa anataka muasisi wetu wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere lakini leo kimekuwa hivyo", amesema Afande Sele.

Pamoja na hayo, Afande sele ameendelea kwa kusema "naomba nikupongeze sana kwa hilo lakini kama haitoshi naomba nikuhakikishie kwamba leo hii kutoka kwa dhati ya moyo wangu nimeamua nisimame upande mmoja na wewe ili nisiachwe katika maendeleo. Ninaamini kabisa Mhe. Rais sasa hivi Tanzania kama gari basi dereva ametulia na gari linakwenda na mimi kama abiria niachwe ninywe soda yangu kwa amani kwasababu naamini kabisa chombo chetu kinaenda sehemu salama na sipendi kesho historia ije kunihukumu kwa watu wale ambao hawakuchangia walichonacho katika kufikisha mahali kinapoenda".

"Nawaomba viongozi ngazi ya mkoa wa CCM mnipokee kijana wenu nije kuongeza nguvu", amesisitiza Afande sele.

Kwa upande mwingine,  Afande Sele aliwahi kugombea Ubunge Jimbo la Morogoro Mjini mwaka 2015 kupitia chama cha ACT Wazalendo kabla ya kujivua uanachama na kusema kuwa hataki tena kujihusisha na siasa.

Post a Comment

 
Top